Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikel Obi ampigia chapuo Filipe Luís Chelsea, amkataa Fabregas

OBI Pict

Muktasari:

  • Nafasi hiyo ya kocha mkuu pale Stamford Bridge iko wazi kufuatia kuondoshwa kwa Rosenior wiki iliyopita baada ya mfululizo wa matokeo mabaya, ambapo kwa sasa timu hiyo inaongozwa na kocha wa muda, Calum McFarlane.

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, John Mikel Obi, ameushauri uongozi wa klabu ya Chelsea kumteua Filipe Luís, kuwa kocha mpya wa timu hiyo ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Liam Rosenior.

Nafasi hiyo ya kocha mkuu pale Stamford Bridge iko wazi kufuatia kuondoshwa kwa Rosenior wiki iliyopita baada ya mfululizo wa matokeo mabaya, ambapo kwa sasa timu hiyo inaongozwa na kocha wa muda, Calum McFarlane.

Akizungumza kupitia podcast yake, Mikel Obi ameeleza kuwa amevutiwa na uwezo wa ufundishaji wa Filipe Luís, hasa kutokana na falsafa yake ya soka aliyoionesha hivi karibuni.

"Kuhusu Filipe Luís, yeye ni kocha mzuri sana. Timu yake ilicheza soka la kuvutia katika Kombe la Dunia la Klabu na walikuwa na malengo ya namna walivyotaka kucheza," amesema Mikel.

OB 02

Ameongeza kuwa, Luís ana sifa za kuwa kocha bora duniani akibainisha kwamba: "Kulikuwa na muundo wa wazi, kucheza kwa malengo, hivyo ndivyo unavyomtambua mtu anayeweza kuwa kocha wa kiwango cha juu."

Licha ya majina ya makocha kama Cesc Fabregas na Andoni Iraola kuhusishwa na matajiri hao wa London Magharibi, Mikel anaamini kuwa Fabregas bado anahitaji muda zaidi wa kukomaa kabla ya kupewa jukumu hilo zito.

OB 01

"Nadhani kwangu itakuwa ni mapema mno kwa Fabregas. Labda hata kwa Luís ni mapema, lakini kati ya makocha watatu wanaotajwa, kama wataamua kwenda na mmoja wapo, mimi nitaenda na Filipe Luís," amesisitiza kiungo huyo wa zamani wa Chelsea.

Chelsea kwa sasa inapitia kipindi cha mpito huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona mmiliki wa klabu hiyo atamteua nani kuinusuru timu hiyo iliyopoteza mwelekeo chini ya Rosenior.

Calum McFarlane anatarajiwa kuendelea kuongoza kikosi hicho hadi mchakato wa kumpata kocha mpya utakapokamilika.