Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fabregas ruksa kwenda Chelsea

FABREGAS Pict

Muktasari:

  • Fàbregas, aliyewahi kushinda Ligi Kuu England mara mbili akiwa na Chelsea kama mchezaji, anachukuliwa kama mmoja wa makocha vijana wenye mvuto mkubwa duniani kwa sasa, hasa kutokana na falsafa yake ya soka ya timu kumiliki mpira muda mwingi.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Como, Cesc Fabregas ambaye anatajwa kuwa mmoja kati ya makocha wanaoweza kuchukua nafasi ya kuifundisha Chelsea baada ya kuondoka kwa Liam Rosenior, amepewa ruhusa ya kuondoka na mabosi wa Como ambao wamesema uamuzi upo mikononi mwake.

Akizungumza na chombo cha habari cha City AM, rais wa klabu ya Como, Mirwan Suwarso amesema: "Kama hiyo itamfurahisha, basi uamuzi ni wake anaweza kuondoka. Sisi tunamsikiliza yeye ikiwa angependa kufanya kazi hapa au kuondoka ni yeye tu, lakini hatummiliki yuko huru kwenda Chelsea kama atataka.”

Hata hivyo, Fabregas mwenyewe amepunguza presha ya uvumi huo na kuweka wazi kwa sasa hana mpango wa kuondoka.

"Sina cha kusema kuhusu hilo. Itakuwa ujinga kufikiria hilo kwa sasa. Akili yangu iko kwenye mechi ijayo dhidi ya Genoa.”

Aliendelea: "Ninaamini nitaendelea kuwepo Como kama kocha mkuu. Nitakuwa na wazimu kama nitafikiria kitu kingine badala ya mechi hizi tano zilizobaki na kujaribu kuipeleka timu kucheza michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia.”

Kocha huyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa Arsenal, Chelsea na FC Barcelona aliichezea Como mwaka 2022 kabla ya kuhamia kwenye benchi la ufundi mwaka 2023.

Aliisaidia timu kupanda daraja kutoka Serie B hadi Serie A na sasa wanapambana kufuzu Ligi ya mabingwa Ulaya wakiwa wanashikilia nafasi ya tano kwa sasa.

Fàbregas, aliyewahi kushinda Ligi Kuu England mara mbili akiwa na Chelsea kama mchezaji, anachukuliwa kama mmoja wa makocha vijana wenye mvuto mkubwa duniani kwa sasa, hasa kutokana na falsafa yake ya soka ya timu kumiliki mpira muda mwingi.