Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikel Arteta hajamaliza kusajili mjue!

Muktasari:

  • Hilo linaiacha Arsenal kwenye mashaka makubwa ya kufanya usajili wa pesa nyingi kwenye dirisha hili kabla halijafungwa la kama itauza kwanza.

LONDON, ENGLAND: KOCHA Mikel Arteta bado anataka kuboresha kikosi chake kwenye wingi ya kushoto, lakini atahitaji kupiga bei mastaa kadhaa ili kuweza kusajili.

Hilo linaiacha Arsenal kwenye mashaka makubwa ya kufanya usajili wa pesa nyingi kwenye dirisha hili kabla halijafungwa la kama itauza kwanza.

Arsenal imekuwa ikihusishwa na supastaa wa Real Madrid, Rodrygo wakati Arteta ni shabiki mkubwa wa staa wa Crystal Palace, Eberechi Eze, lakini wote hao wawili hakuna anayepatikana kwa gharama ndogo.

Na sasa, Tottenham ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa Eze baada ya mazungumzo kwenda vizuri kwenye dili la Pauni 60 milioni, ambapo Pauni 55 milioni itatangulizwa na Pauni 5 milioni italipwa kama bonasi, huku Palace ikikomaa ili kufanya biashara nzuri.

Arsenal kwa sasa bajeti imebana kutokana na kutumia zaidi ya Pauni 200 milioni kwenye usajili wa dirisha hili, jambo linalomfanya mkiyrugenzi wa michezo, Andrea Berta kupambana kuweka mambo sawa.

Winga Leandro Trossard anahusishwa na klabu za Brentford, Aston Villa na timu za nje huko baada ya sasa kuweka chini kabisa kwenye chaguo la kupata namba kwenye timu. Wachezaji wenzake kwenye kikosi cha Arsenal, Jakub Kiwior, Oleksandr Zinchenko, Fabio Vieira, Albert Sambi Lokonga na Reiss Nelson ni wachezaji wengine ambao wapo njiani kuachana na timu hiyo dirisha hili.

Kinda Max Dowman, 15, aliichwa nje kwenye mechi iliyopita, wakati Christian Norgaard alipata matatizo ya majeraha na Gabriel Jesus bado hajapona sawasawa maumivu yake ya enka.

Fenerbahce imeonyesha dhamira ya kumsajili Zinchenko, ambaye mkataba wake umebakiza mwaka mmoja, wakati Porto na Stuttgart zinazo zinahitaji saini ya Vieira. Lokonga naye kuna timu zinamtaka, wakati Kiwior, naye anafikiria kuondoka kwenye timu hiyo kutokana na kukosa nafasi kikosini Arsenal. Arsenal ilimsajili winga Noni Madueke kutoka Chelsea kwa Pauni 52 milioni, kati Gabriel Martinelli alicheza kwenye mechi ya Old Trafford na bila shaka ataendelea kupata nafasi kikosini. Lakini, kwa Arsenal kuhitaji saini ya Eze hilo litakwenda kuweka kikwazo kwa Ethan Nwaneri na Dowman katika kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Arteta.