Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mieleka ya vidole vya miguu

MIELEKA Pict

Muktasari:

  • Mchezo huo umejizolea umaarufu mkubwa Ulaya na umekuwa na mashindano ya dunia yanayofanyika kila mwaka. Lakini huwa unachezwaje? Hapa tunakupa maelezo wa kina kuanzia kanuni, unavyochezwa na historia.

DUNIANI kuna michezo mingi ambayo imekuwa na mashabiki wanaopenda kuitazama. Mojawapo kati ya michezo hiyo ni ule wa mieleka ya kupigana kwa vidole vya miguu ambao ulianzishwa huko Uingereza.

Mchezo huo umejizolea umaarufu mkubwa Ulaya na umekuwa na mashindano ya dunia yanayofanyika kila mwaka. Lakini huwa unachezwaje? Hapa tunakupa maelezo wa kina kuanzia kanuni, unavyochezwa na historia.

MIE 04

HISTORIA

Mchezo huu ulianzishwa katika Mji wa Wetton, Derbyshire, Uingereza mwaka 1974 na kikundi  cha wenyeji waliokuwa wakiendelea kunywa pombe kwenye baa, na walijadili kuanzisha mchezo ambao wangeweza kushindana nao kwani hawakuwa wazuri katika michezo mingine.

Mashindano ya kwanza ya kupigana kwa vidole vya miguu yalifanyika maeneo ya Derbyshire katika baa ndogo na tangu hapo yakapata umaarufu na watu kutoka nchi mbalimbali wakawa wanaucheza na sasa unaonyeshwa hadi katika vyombo vya habari.

Mwaka 2006, kampuni ya ice-cream ya Ben & Jerry’s ilinunua nembo ya biashara ya mchezo huu na kudhamini mashindano. Hata hivyo, mwaka 2016, Alan Nash, bingwa wa zamani alinunua nembo hiyo na tangu wakati huo amefanya kazi ya ziada kuhakikisha mchezo unakua zaidi.

MIE 01

JINSI UNAVYOCHEZWA

Washindani wawili hupigana kwenye jukwaa maalum linaloitwa “toedium” ambalo lina kuta mbili, kulia na kushoto kisha, washindani husika wataweka miguu katika uwazi uliopo katikati.

Baada ya hapo huku wakiwa wanaangaliana, kila mmoja atagusishwa vidole vya miguu yake na vya mwenzake na kumlazimisha mpinzani kugusa ukuta mmoja wapo ambao atakuwa ameuchagua wakati mchezo unaanza kama ndio goli lake.

 Washindani wanapaswa kushikilia vidole vya miguu vya mpinzani ili kufanikisha hilo ambapo watatakiwa kutumia nguvu, mbinu, na uvumilivu.

Kawaida, mechi  inachezwa katika mfumo wa raundi tatu na  mtu wa kwanza kushinda mizunguko miwili ndiye mshindi.

Hakuna muda kamili uliowekwa juu ya ukomo wa raundi, hivyo washindani wanaweza kushindana hadi saa mbili hadi mmoja ashinde.

MIE 02

KANUNI

Kwa kuwa wachezaji hupigana kwa vidole vya miguu hali inayohusisha kugusana kwa miguu ya washindani, usafi ni muhimu sana. Washindani watakaguliwa kuhakikisha miguu yao ni safi na hawana maambukizi au vidonda.

 Majeraha kama vile kuvunjika kwa vidole, vidonda, au maumivu ya magoti yanaweza kutokea wakati wa mashindano.

MIE 03

MAMBO YA KUVUTIA

Mshindi wa mashindano ya dunia katika mchezo huu hupokea tuzo ya mguu wa shaba na hufanyika kila mwaka kuanzia Agosti katika baa ya Haig huko Derbyshire, Uingereza.

Bingwa mara nyingi wa dunia katika michezo hii ni Alan ‘Nasty’ Nash, ambaye ameshinda mara 17 na bingwa mtetezi hadi sasa ni Ben Woodroffe.