Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi aweka rekodi mpya Marekani

Muktasari:

  • Akiwa na umri wa miaka 38, Messi anaonekana kufurahia kiwango bora zaidi tangu alipowasili Marekani, huku Inter Miami tayari ikiwa imefuzu kwa hatua ya mtoano ya MLS, na sasa inapambana kuboresha nafasi yake kwenye msimamo kabla ya hatua ya mwisho ya msimu.

Lionel Messi anaendelea kuthibitisha kuwa mchango wake katika Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS) hauna kifani. Katika mchezo dhidi ya New England Revolution, nahodha huyo wa Inter Miami alitoa asisti tatu na sasa amehusika kwenye mabao 40 msimu wa 2025. Lakini zaidi ya ushindi huo, Messi sasa amehusika kwenye mchango wa mabao 100 akiwa na Inter Miami akifunga 66 na asisti 34 katika mechi 80 pekee.

Akiwa na umri wa miaka 38, Messi anaonekana kufurahia kiwango bora zaidi tangu alipowasili Marekani, huku Inter Miami tayari ikiwa imefuzu kwa hatua ya mtoano ya MLS, na sasa inapambana kuboresha nafasi yake kwenye msimamo kabla ya hatua ya mwisho ya msimu.


ANAITAFUTA REKODI YA CARLOS VELA

Kilichopo mbele ya Messi ni kuvunja rekodi ya Carlos Vela, ambaye mwaka 2019 akiwa na Los Angeles FC

nayo sasa, Messi anaweza kufikia au hata kuvunja rekodi hiyo kabla ya msimu wa kawaida kumalizika, hasa ikiwa Inter Miami itafika hatua za mwisho za ligi.

Timu hiyo inayoongozwa na Javier Mascherano inamtegemea Messi zaidi kuliko wakati wowote ule. Baada ya kutolewa kwenye Leagues Cup dhidi ya Seattle Sounders, nguvu zote sasa zimeelekezwa katika kutwaa ubingwa wa MLS, taji pekee ambalo Messi hajashinda tangu afike Marekani.

Mbali na rekodi za ndani, Messi pia yuko karibu kufikia asisti 400 katika soka. Asisti tatu alizotoa wikendi sasa amefikisha 395, hakuna mchezaji mwingine wa sasa aliyeikaribia hata kwa kufikisha 300. Hii inaonyesha ukubwa wa mafanikio ya nyota huyo wa Argentina.

Mchango wake unaonyesha si tu ubora wake binafsi, bali pia uwezo wake mkubwa wa kuzoea soka la Marekani. Katika ligi inayozidi kuwa na ushindani mkali, Messi ameibadilisha Inter Miami kuwa timu tishio na kuongeza umaarufu wa mchezo huo nchini Marekani.


ORODHA YA WENYE ASISTI NYINGI

1. Lionel Messi – 400

2. Luis Figo – 283

3. Neymar – 280

4. David Beckham – 272

5. Ryan Giggs – 271

6. Cristiano Ronaldo – 257

7. Thierry Henry – 246

8. Luis Suárez – 243

9. Thomas Müller – 242

10. Franck Ribéry – 241