Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa hawa wametisha kwa mabao karne ya 21

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Ni hivyo pia yanapotajwa majina ya wakali kama Kylian Mbappe, Viktor Gyokeres, Robert Lewandowski, Benjamin Sesko, Victor Osimhen na Raphinha. Ni mabao tu.

LONDON, ENGLAND: LINAPOTAJWA jina la Erling Haaland, kinachokujua akilini kwa haraka ni mabao.

Ni hivyo pia yanapotajwa majina ya wakali kama Kylian Mbappe, Viktor Gyokeres, Robert Lewandowski, Benjamin Sesko, Victor Osimhen na Raphinha. Ni mabao tu.

Lakini, kuna wakali hao ni balaa zaidi kwenye ishu ya kuhusika kwenye mabao mengi, kwa maana ya kufunga na kuasisti katika karne ya 21. Kuna nyota wengi wa kutoka klabu za Barcelona, Bayern Munich na Real Madrid, wametisha kwa kufunga.

Kufunga mabao ni kitu muhimu sana katika mchezo wa soka na wachezaji waliopo kwenye orodha hii si hodari tu kwenye kutumbukia mipira kwenye nyavu za magoli ya wapinzani, bali pia ni mahiri katika kuwatengenezea wenzao nafasi za kufunga kwa maana ya kuwapigia pasi za mwisho.

Kwa kujumuisha mabao ya klabu na timu ya taifa, hii hapa orodha ya wanasoka saba ambao wamehusika kwenye mabao mengi ndani ya karne hii ya 21.

MASTA 07

7. Neymar – 656 mabao + asisti

Mchezaji huyo ameshindwa kucheza kwa kiwango kikubwa tangu alipofikisha umri wa miaka 30, lakini kinachovutia ni wa kwamba Neymar alionyesha kiwango bora cha kufunga wakati alipokuwa na umri mdogo.

Kwa mabao yake ya klabu na timu ya taifa, wastani wake wa mchango wa mabao ni 0.89 kwa kila mechi, rekodi inayomfanya kuwa miongoni mwa mastaa matata kabisa. Neymar mambo yake si mazuri kwa sasa, lakini akitazama rekodi zake bila shaka anafarijika.

MASTA 06

6. Karim Benzema – 689 mabao + asisti

Kwenye orodha hii ya wakali wa kufunga na kuasisti kinachoshangaza ni wachezaji watatu tu ndiyo waliowahi kushinda tuzo ya Ballon d’Or.

Mmoja wa mastaa hao ni Benzema, aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2022 shukrani kwa kile alichofanya Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Licha ya kutumikia kipindi cha ubora wa soka lake akiwatengenezea mabao wengine, takwimu zake kwenye kufunga na kuasisti bado ziliendelea kuwa bora na kwenye kikosi cha Madrid alichangia mabao 509 na bado anaendelea kufunga huko kwenye kikosi cha Al-Ittihad.

MASTA 05

5. Zlatan Ibrahimovic – 726 mabao + asisti

Ibrahimovic alianza maisha yake ya soka la kulipwa 1999, lakini sehemu kubwa ya mabao yake ilikuwa kwenye karne ya 21.

Fowadi huyo wa Sweden amefunga mabao kwenye nchi saba tofauti kwenye ngazi ya klabu, akitamba kwenye vikosi vya Paris Saint-Germain, AC Milan na Inter Milan.

Katika kipindi cha soka lake, Ibrahimovic amekuwa na wastani wa mchango wa mabao wa 0.74 kwa mechi, baada ya kuhusika kwenye mabao 726 kwa maana ya kufunga na kuasisti katika mechi 980.

MASTA 04

4. Luis Suarez – 836 mabao + asisti

Katika kipindi cha ubora wa soka lake, hakuna mtu anayepinga Luis Suarez alikuwa mmoja wa mastraika matata kabisa kwenye kizazi chake.

Staa huyo wa Uruguay alikuwa kiboko ya makipa kwenye timu alizochezea na alitamba na klabu za Liverpool na Barcelona, akishinda tuzo mbalimbali za kuwa kinara wa mabao.

Kwa sasa akiwa na umri wa miaka 38, bado anaendelea kuongeza idadi yake ya mabao akiwa kwenye kikosi cha Inter Miami huko Marekani.

MASTA 03

3. Robert Lewandowski – 841 mabao + asisti

Straika Lewandowski bado anaendelea kukomaa kwa maana ya kuendelea kucheza, ambako huko kwenye kikosi cha Barcelona amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake kwenye ishu ya kufunga mabao licha ya sasa kuwa na umri wa miaka 37.

Straika huyo wa Poland, sehemu kubwa ya mchango wake wa mabao amefunga akiwa na vikosi vya Borussia Dortmund na Bayern Munich huko Ujerumani kabla ya sasa kufanya mambo yake kwenye kikosi cha Barcelona huko Hispania.

Bado ni hatari sana anaposogelea goli la wapinzani, ambapo sasa anakaribia mabao 900 kwenye mchango wake wa kufunga na kuasisti.

MASTA 01

2. Cristiano Ronaldo – 1,195 mabao + asisti

Wakati Ronaldo anaanza soka alikuwa akifahamika zaidi kwa kasi yake, ufundi na winga machachari kabla ya kuhamia katikati ya uwanja, mbele ya goli na kuwa mtambo wa kuzalisha mabao.

Ndiye kinara wa kufunga mabao kwenye karne ya 21, akitikisa nyavu zaidi ya 938, akiendelea na kampeni yake ya kufikisha mabao 1000 ya kufunga. Lakini, staa huyo wa Kireno si mchoyo pia katika kutengenezea wenzake nafasi za kufunga na ameasisti 257 na hivyo kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wamechangia mabao mengi katika karne hii ya 21.

MASTA 02

1. Lionel Messi – 1,264 mabao + asisti

Ni nani mwingine kama si supastaa Lionel Messi? Muargentina huyo anashika namba moja kwenye orodha ya wanasoka waliochangia mabao mengi kwa maana ya kufunga na kuasisti katika karne ya 21.

Katika mechi 1,117, Messi amechangia mabao 1,264 na kumfanya kuwa mchezaji pekee kwenye wastani chanya.

Kwa kutafuta mchanganuo huo wa mabao, Messi amefunga mara 875, huku mabao 666 akifanya hivyo kwenye kikosi cha Barcelona, ambako pia aliasisti mara 389.

Msimu wake bora ulikuwa wa 2011-12, wakati alipofunga mabao 73 katika michuano yote, wakati mwaka 2012, alifunga mabao 91 ndani ya mwaka mmoja.