Messi awapa hasara mashabiki

MIAMI, MAREKANI. MAELFU ya mashabiki wa Lionel Messi wamepigwa na butwaa baada ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kumuona staa wao huko Atalanta kabla ya mechi yao, hata hivyo alibaki Miami huku Inter Miami ikipokea kichapo cha mabao 5-2 dhidi ya Atalanta United.

Kuelekea mchezo wa Inter Miami na Atalanta United kabla ya kuchezwa maelfu ya jezi za pinki za Messi zilienea nje ya uwanja hata hivyo staa huyo hakucheza kutokana na kuwa majeruhi.

Gazeti la Dail Mail ilizungumza na mashabiki waliokuwa nje ya Uwanja wa Mercedes-Benz, wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 73,000 walidai walisafiri umbali mrefu kwa ajili ya kumuona Messi bila kujua kwamba hakujumuishwa kikosini.

Familia moja iliendesha gari masaa 10 kutoka Florida Kusini kwa ajili ya mechi hiyo huku mashabiki wengine wakinunua tiketi za gharama kwa ajili ya mechi hiyo ya ligi.

Awali ilitarajiwa Messi angecheza mechi hiyo lakini picha ziliibuka mtandaoni zikimuonyesha yupo bize akimuangalia mtoto wake akiichezea timu ya vijana ya Inter Miami.