Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi akosa penalti, Argentina ikitinga nusu fainali Copa America

Muktasari:

  • Kipute hicho cha robo fainali kimepigwa leo alfajiri katika Uwanja wa NRG mjini Houston, Texas huko Marekani.

TEXAS, MAREKANI. Uzoefu wa kikosi cha Argentina umekisaidia kutinga nusu fainali ya mashindano ya mataifa ya Amerika (Copa America) baada ya kuifunga Ecuador kwa mikwaju ya penati 4-2.

Kipute hicho cha robo fainali kimepigwa leo alfajiri katika Uwanja wa NRG mjini Houston, Texas huko Marekani.

Timu hizo zilifikia hatua ya mikwaju ya penati baada ya kufungana bao 1-1 katika dakika 120 za mchezo.

Nahodha na mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi alikosa penati ya kwanza huku Álvarez, Mac Allister, Montiel na Otamendi wakifanikiwa kukwamisha zao nyavuni.

Upande wa Ecuador, Mena na Minda walikosa penati za awali, lakini Yeboah na Moisés Caicedo wakifanikiwa kufunga walizopiga.

Katika muda wa kawaida Argentina ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Lisandro Martínez katika dakika ya 35, lakini Ecuador ilifanikiwa kusawazisha dakika ya 90 kupitia kwa Kevin Rodríguez.

Robo fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi kati ya Venezuela dhidi ya Canada katika uwanja wa AT&T mjini Arlington, Texas.

Argentina yatinga nusu fainali Copa America, Messi akosa penati

Uzoefu wa kikosi cha Argentina umeisaidia timu hiyo kutinga nusu fainali ya Copa America baada ya kuifunga Ecuador kwa mikwaju ya Penati 4-2, katika mchezo wa robo fainali uliopigwa leo alfajiri katika uwanja wa NRG mjini Houston, Texas huko Marekani.

Timu hizo zilifika hatua ya mikwaju ya Penati baada ya kufungana 1-1 katika dakika 120.

Nahodha na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi alikosa Penati ya kwanza, huku Álvarez, Mac Allister, Montiel na Otamendi wakifanikiwa kukwamisha Penati zao nyavuni.

Upande wa Ecuador Mena na Minda walikosa Penati za awali, lakini Yeboah na J. Caicedo walifanikiwa kupata.

Katika muda wa kawaida Argentina ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Li. Martínez katika dakika ya 35 lakini Ecuador walifanikiwa kusawazisha dakika ya 90 kupitia kwa Rodríguez.

Robo fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi kati ya Venezuela dhidi ya Canada katika uwanja wa AT&T mjini Arlington, Texas.