Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi za ubingwa Arsenal, Man City hesabu zipo hapa

UBUNGWA Pict
UBUNGWA Pict

Muktasari:

  • Bao la mapema la Bukayo Saka dakika ya tisa, liliwapa Arsenal pointi tatu muhimu, wakati kikosi cha Pep Guardiola kililazimishwa sare ya 2-2 nyumbani dhidi ya Forest.

LONDON, ENGLAND: KATIKATI ya wiki hii, Arsenal iliweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuchukua taji la Ligi Kuu England msimu huu, baada ya kuichapa Brighton & Hove Albion, wakati wapinzani wao Manchester City wakipoteza pointi dhidi ya Nottingham Forest.

Bao la mapema la Bukayo Saka dakika ya tisa, liliwapa Arsenal pointi tatu muhimu, wakati kikosi cha Pep Guardiola kililazimishwa sare ya 2-2 nyumbani dhidi ya Forest.

Antoine Semenyo alifunga bao la kwanza kwa City kabla ya Morgan Gibbs-White kusawazisha. Rodri aliifungia Man City bao la pili, lakini Elliot Anderson alifunga tena na kuisaidia Forest kupata pointi moja muhimu.

Baada ya matokeo hayo, jumla sasa zimebakia mechi nane kwa Arsenal huku Man City ikiwa na tisa na washika mitutu wanaongoza kwa tofauti ya pointi saba.

Ukiondoa mechi za FA Cup zitakazochezwa mwisho wa wiki hii, kuna mechi tano ambazo kwa kiasi kikubwa zinaonekana kuwa zitaamua ni timu gani itachukua ubingwa kati ya Arsenal au Man City.

Katika mechi hizo tano kwa Arsenal, ya kwanza itaanza Machi 14, nyumbani dhidi ya Everton, pia itavaana na  Bournemouth nyumbani, Aprili 11 kisha kutakuwa na mechi ya hukumu kati yao na Man City Ugenini kwenye dimba la Etihad, Aprili 19.

Mechi hii na Man City inaonekana kuwa muhimu zaidi kwa timu zote kwani yoyote itakayopoteza itakuwa imepunguza asilimia kubwa za kuchukua ubingwa.

Vilevile Arsenal itacheza nyumbani dhidi ya Newcastle United Aprili 25 na mechi ya tano kati ya hizo ni dhidi ya  Fulham ambayo pia itapigwa dimba la Emirates, Mei.

Kwa upande wa mechi tano za Man City, ya kwanza itakuwa ni dhidi ya West Ham United ugenini,  Machi 14 kisha itasafiri kwenda London kuvaana na Chelsea Aprili 12 na baada ya hapo itakutana na mechi ya maamuzi dhidi ya Arsenal katika dimba la Etihad ambayo ikipoteza itakuwa imeweka tofauti ya pointi saba na ikishinda itakuwa imeweka tofauti ya pointi moja.

Mechi mbili za mwisho ni dhidi ya Burnley ugenini, Aprili 26 na  Everton ugenini, Mei.

Hata hivyo, kocha wa Brighton, Fabian Hurzeler aliikosoa vikali Arsenal  akidai wanapoteza muda sana jambo ambalo hupoteza ladha ya mechi: "Ninauliza swali moja: Umewahi kuona mechi ya EPL ambayo kipa  anaanguka mara tatu. Sitawahi kuwa kocha wa aina hiyo, tunahitaji kuweka sheria zilizo wazi zaidi, kuwe na kikomo cha kuchelewesha muda, wapo tayari kufanya chochote ili kushinda, mimi sioni kama ni jambo zuri."

Alipoulizwa kwa upande wake Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alijitetea  maoni kama hayo ni mengi lakini hawayaangalii sana."