Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola anang’ata, anapuliza kuhusu kona

Muktasari:

  • Kocha wa Liverpool, Slot, alizua mjadala Jumatatu alipokiri kwamba moyo wake wa soka haupendi utegemezi mkubwa wa mipira ya adhabu msimu huu.

LIVERPOOL, ENGLAND: PEP Guardiola amemwambia Arne Slot kwamba anapaswa kupambana na hali juu ya ongezeko la umuhimu wa mipira ya adhabu katika Ligi Kuu England  huku akipiga kijembe Arsenal kwamba wamekuwa vinara wa mipira hiyo.

Kocha wa Liverpool, Slot, alizua mjadala Jumatatu alipokiri kwamba moyo wake wa soka haupendi utegemezi mkubwa wa mipira ya adhabu msimu huu.

Katika kipindi cha mapumziko kwenye mechi ya ushindi wa kusisimua wa mabao 5-2 dhidi ya West Ham United, Jumamosi, Liverpool ilikuwa imefunga mabao yao saba yaliyotangulia yote kutokana na mipira ya adhabu, ikiwa ni rekodi mpya kwenye Ligi Kuu England.

Mjadala kuhusu mipira ya adhabu uliendelea baada ya ushindi wa mabao 2-1 wa Arsenal dhidi ya Chelsea, Jumapili, ambapo mabao yote matatu yalitokana na kona. Na sasa Guardiola ametoa maoni yake, akisema kwa kiasi fulani anakubaliana na Slot huku akisisitiza kwamba makocha lazima wajifunze kuendana na mabadiliko.

“Mipira ya adhabu imeanza kuwa sehemu muhimu ya mikakati,” alisema kocha huyo wa Manchester City, Guardiola na kuongeza.

“Ilikuwa tofauti nilipoanza kazi ya ukocha. Nilipokuwa kijana, tulisema watu wa Uingereza hushangilia kona na mipira ya adhabu kama bao. Nakumbuka vizuri nilipokuwa mdogo, kwa hiyo hakuna kilichobadilika kwa upande huo.

“Ni kweli Arsenal inaongoza kidogo namna wanavyofanya jambo hilo na lina umuhimu mkubwa. Miaka minne iliyopita katika NBA, mpira wa alama tatu haukuwa ukitumika sana, lakini Golden State Warriors wakiwa na Stephen Curry walianza kupiga alama tatu nyingi na kila mtu akaendana nao, sasa timu nyingi zinafanya hivyo. Ni sehemu ya mabadiliko na mwenendo wa mchezo. Unaweza kukaa na kulalamika lakini lazima uendane na hali. Ni sehemu ya mchezo.

“Najua mchezo unasimama wakati wa mipira ya adhabu, hauna mwendo wa kasi, lakini ni sehemu ya soka. Lazima uendane na hasa namna inavyoendeshwa kwenye Ligi Kuu England. Kila nchi ina mtindo wake na kila klabu ina namna yake ya kucheza kulingana na kocha na timu. Ninaelewa kabisa sababu ya Arne kusema hivyo na kwa baadhi ya mambo nakubaliana naye.”