Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta: soka la kuvutia ni gumu England

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Arsenal alijibu ukosoaji unaoelekezwa timu yake, ambayo imefunga mabao 24 mengi kuliko timu nyingine yoyote kutokana na mipira ya adhabu na kona msimu huu. Arteta alisema sheria zinapaswa kubadilishwa iwapo mashabiki wanataka burudani zaidi.

LONDON, ENGLAND: MIKEL Arteta anadai kuwa haiwezekani kucheza soka la kuvutia kwenye Ligi Kuu England.

Kocha huyo wa Arsenal alijibu ukosoaji unaoelekezwa timu yake, ambayo imefunga mabao 24 mengi kuliko timu nyingine yoyote kutokana na mipira ya adhabu na kona msimu huu. Arteta alisema sheria zinapaswa kubadilishwa iwapo mashabiki wanataka burudani zaidi.

Lakini, Fabian Hurzeler, ambaye timu yake ya Brighton iliikaribisha Arsenal usiku wa Jumatano, anaamini wanaowania ubingwa wanapoteza fedha za mashabiki wanaoingia uwanjani kwa kutumia zaidi ya dakika moja kupiga kona.

Arteta alisema: “Ningependa kucheza nikiwa na wachezaji watatu wa ziada katika nusu yangu ili kupata soka zuri. Kama unataka kutazama aina hiyo ya soka, lazima uende nchi nyingine kwa sababu katika Ligi Kuu England kwa misimu miwili au mitatu iliyopita, hali si hiyo.”

Kiungo wa Arsenal, Declan Rice alikuwa na bahati kuepuka kusababisha penalti dhidi ya Chelsea, huku Arsenal ikinufaika na uamuzi wa huruma wa waamuzi kuunda nafasi katika mipira ya adhabu ya kushambulia msimu huu.

Arteta aliongeza: “Utakuwa mchezo tofauti isipokuwa tubadilishe sheria. Zamani ulipokuwa unatengeneza mpango wa mchezo, ungeweza kumrudisha beki pembeni ndani, kuongeza mchezaji katikati au kutumia namba tisa wa uongo. Miaka minne iliyopita ulikuwa mchezo tofauti kabisa.” Kwenye hilo la kona, kocha wa Brighton, Hurzeler, alisema: “Wakati Arsenal wanapata kona na wanaongoza, wakati mwingine wanatumia zaidi ya dakika moja kupiga. Kwa hiyo tunapaswa kuwa na sheria zilizo wazi. Kila shabiki anayelipa fedha nyingi kuingia uwanjani anapaswa kuona muda sawa wa mpira ukiwa unachezwa. Wanataka kuona tukio la soka, hawataki kuona labda dakika 50 mpira ukiwa unachezwa na dakika 40 mchezo umesimama.”

Arsenal imefunga mabao 32 kutokana na kona, mipira ya adhabu na mipira ya kurusha kutoka pembeni katika mashindano yote na kwenye hilo, Arteta aliongeza: “Ninakereka kwamba hatufungi mabao zaidi kutokana na mipira hiyo. Nilikerwa sana na namna tulivyofungwa dhidi ya Chelsea. Angalia idadi ya mabao wanayofunga kutokana na mipira ya adhabu. Manchester United inafanya vizuri sana. Nilipokuwa Manchester City tulikuwa tunafanya kazi kubwa sana kwenye mipira hiyo.”

Kocha wa Man United, Michael Carrick, ametoa wito kwa uongozi wa Ligi Kuu England kudhibiti tabia ya kushikana sana ndani ya eneo la penalti wakati wa kupiga kona au mipira ya adhabu kuelekea eneo hilo, alisema: “Si muda mrefu tuliambiwa huwezi kumgusa mtu yeyote ndani ya boksi na tukaambiwa itadhibitiwa. Polepole imerudi tena. Mafanikio ya mabao ya kona na uwezo wa kuweka miili karibu yamefanya timu nyingi kuiga. Haionekani kama tumepata uwiano sahihi.”

Ruud Gullit, aliyebuni kauli ya “sexy football” alipokuwa kocha mchezaji wa Chelsea mwishoni mwa miaka ya 1990, alisema hafurahishwi na soka la Ligi Kuu England kwa sasa, aliposema: “Sijafurahia kutazama soka hata kidogo hivi karibuni. Niliangalia Arsenal dhidi ya Chelsea Jumapili na ulikuwa mchezo mbaya sana. Soka lilikuwa baya kulitazama.”