Mechi za nyumbani Spurs inaomba dua zenu jamani!
Muktasari:
- Unajua kwa nini? Spurs imekuwa na kiwango kibaya sana ikiwa nyumbani msimu huu na si kwa viwango vya Ligi Kuu England pekee.
LONDON, ENGLAND: MCHEZA kwao hutuzwa. Lakini, wahenga wa Tottenham Hotspur wanaangaliana usoni huu ya msemo huo wa kihenga.
Unajua kwa nini? Spurs imekuwa na kiwango kibaya sana ikiwa nyumbani msimu huu na si kwa viwango vya Ligi Kuu England pekee.
Timu hiyo imekuwa nyepesi zaidi kwa wapinzani wao inapocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani, ambao umejengwa kisasa kabisa.
Spurs ilipoteza tena nyumbani Alhamisi usiku, kwa namna iliyo ya kawaida kabisa kwa timu hiyo inapocheza kwenye uwanja wake msimu huu.
Mchezo ulianza vizuri, huku kikosi cha Igor Tudor kikionekana kuwa na dakika mbili bora zaidi za msimu wao katika kipindi cha kwanza dhidi ya Crystal Palace. Waliepuka kuruhusu bao la kwanza pale Ismaïla Sarr aliponaswa kwenye mtego wa kuotea, kabla ya Dominic Solanke kuipatia Spurs bao la kuongoza.
Lakini, dakika tatu baadaye, mambo yalibadilika vibaya kwa Spurs. Nahodha wao na mchezaji muhimu zaidi, Micky van de Ven, alitolewa kwa kadi nyekundu, jambo lililosababisha kuporomoka kwa timu hiyo. Spurs wakitoka kuongoza dakika ya 38 hadi kuwa nyuma kwa mabao 3–1 huku pia wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja kufikia mapumziko ya kipindi cha kwanza.
Kwa baadhi ya mashabiki wa Spurs, hilo lilitosha kuwafanya kuondoka uwanjani mapema. Na kwa kuzingatia kiwango kibaya sana walichokiona katika Uwanja wa Tottenham Hotspur msimu huu, ni nani angewalaumu?
Ikiwa jambo lisilofikirika litatokea na Spurs ikashuka daraja, rekodi ya mbaya ikiwa nyumbani itakuwa moja ya sababu kuu pamoja na kushindwa kwao kushinda mechi popote walipo katika mwaka wa 2026.
Spurs imekusanya pointi 10 tu katika mechi 15 ilizocheza nyumbani msimu huu, ikipoteza mechi tisa kati ya hizo. Ni tofauti ya mabao pekee inayowazuia kuwa na rekodi mbaya zaidi katika Ligi Kuu England.
Katika klabu zote 92 za EFL Championship, EFL League One na EFL League Two, ni Sheffield Wednesday pekee iliokusanya pointi chache zaidi nyumbani kuizidi Spurs. Na klabu hiyo ya Owls ilionekana tayari iko hatarini kushuka daraja kutoka Championship hata kabla msimu haujaanza, wakati Thomas Frank bado alikuwa na matumaini makubwa kuhusu msimu ujao.
Barani Ulaya, katika ligi tano kubwa, ni klabu za Hellas Verona, Pisa SC, FC Metz, FC Nantes na VfL Wolfsburg pekee ambazo zimepata pointi chache zaidi nyumbani.
Hata hivyo, zote zimecheza mechi chache za nyumbani kuliko Spurs, na ni Pisa pekee inaoweza kulingana na Spurs kwa kupoteza mechi tisa nyumbani. Spurs bado ina mechi nne za nyumbani zilizobaki katika Ligi Kuu England; mechi muhimu dhidi ya Nottingham Forest, Leeds United, Brighton na Everton.
Forest, Brighton na Everton zote zimekusanya pointi nyingi zaidi zikiwa ugenini kuliko Spurs walizopata nyumbani, wakati rekodi ya Leeds ugenini kwa sasa inalingana na rekodi ya Spurs inapocheza nyumbani. Takwimu hizo si habari njema kabisa kwa Spurs na rekodi yake katika mechi za nyumbani ilizocheza msimu huu kwenye Ligi Kuu England.
MSIMAMO WA MECHI ZA NYUMBANI LIGI KUU ENGLAND
P W D L GF GA GD PTS
1.Man City 15 11 3 1 36 11 +25 36
2.Arsenal 14 11 2 1 33 9 +24 35
3.Man United 14 9 3 2 27 16 +11 30
4.Aston Villa 15 9 2 4 21 15 +6 29
5.Liverpool 14 8 3 3 26 16 +10 27
6.Sunderland 14 7 5 2 22 13 +9 26
7.Fulham 15 8 2 5 24 18 +6 26
8.Newcastle 15 8 2 5 28 24 +4 26
9.Brentford 14 7 4 3 24 15 +9 25
10.Bournemouth 15 6 7 2 21 15 +6 25
11.Brighton 15 6 6 3 22 16 +6 24
12.Chelsea 14 6 5 3 23 16 +7 23
13.Leeds 15 6 4 5 22 20 +2 22
14.Everton 15 5 4 6 18 19 -1 19
15.Crystal Palace 14 3 6 5 14 18 -4 15
16.Nottm Forest 14 3 4 7 13 19 -6 13
17.West Ham 14 3 3 8 17 27 -10 12
18.Wolves 16 3 3 10 17 31 -14 12
19.Tottenham 15 2 4 9 18 25 -7 10
20.Burnley 14 2 4 8 15 23 -8 10