Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi tisa zaleta shida Man City

MAN CITY Pict

Muktasari:

  • Na kwamba Man City yenyewe imekiri kufanya makosa hayo na hivyo italazimika kulipa faini hiyo.

LONDON, ENGLAND: MANCHESTER City imekumbana na adhabu ya kupigwa faini ya Pauni 800,000 baada ya kufanya makosa kwenye mechi tisa za Ligi Kuu England kwa kuvunja kanuni za mchezo.

Na kwamba Man City yenyewe imekiri kufanya makosa hayo na hivyo italazimika kulipa faini hiyo.

Kanuni ya Ligi Kuu England inayofahamika kama Rule L.33, inaeleza kwamba timu zote za Ligi Kuu England hazipaswi kuchelewesha kuanzishwa kwa mchezo iwe ni mwanzo au baada ya mapumziko, kwa maana kwamba inapaswa kuwahi uwanjani au sivyo itakupambana na adhabu ya kutozwa faini.

Faini hiyo itapanda kila baada ya kosa, ambapo kwa kosa la kwanza timu itatakiwa kulipa Pauni 40,000, hivyo kwa kosa la tisa timu itakuwa imefikia kutozwa faini ya Pauni 190,000.

Taarifa ya Ligi Kuu England ilisomeka hivi: “Ligi Kuu na Manchester City FC zimefikia kwenye makubaliano baada ya klabu hiyo kukubali kuvunja kanuni ya ligi L.33 inayohusiana na muda wa kuanza mechi mwanzoni na pale baada ya mapumziko. Makosa hayo yamefanyika kwenye mechi tisa za Ligi Kuu England msimu wa 2024/25. Kanuni hiyo imewekwa ili kuzifanya timu kuwa profesheno kwa maana ya kuheshimu muda ili kuhakikisha matangazo ya mechi zote za Ligi Kuu England kuwa kwenye ratiba sahihi.”

Miongoni mwa mechi hizo tisa ambazo Man City ilivunja kanuni ya Rule L.33 ni ile ya kichapo cha kwenye Manchester derby, ilipokung’utwa na Man United uwanjani Etihad, Desemba mwaka jana.

Katika mechi hiyo, Man City ilichelewesha mchezo katika kipindi cha kwanza na baada ya mapumziko.

Kanuni ya Rule L.33 inasemaje?

“Klabu yoyote, bila sababu yoyote, ikisababisha kuchelewa kuanza kwa mechi ya Ligi Kuu kwa muda uliopangwa au kuchelewesha kuanza kwa mechi baada ya mapumziko itawajibishwa.”

Na kwenye hilo, Ligi Kuu England ilithibitisha kwamba Man City imeomba radhi kwa kutenda makosa. Na makocha wa klabu hiyo ya Etihad wamewaambia wachezaji na makocha wao kuhakikisha wanawajibika kwa kuzingatia kanuni hiyo ya Rule L.33.