Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi mpya FA, mpira mpya

Mpira FA Pict

Muktasari:

  • Safari hii miamba hiyo itakutana kwenye mchezo wa Raundi ya Tatu ya Kombe la FA huko uwanjani Emirates.

LONDON, ENGLAND: KIPUTE cha Arsenal na Manchester United kitapigwa keshokutwa, Jumapili.

Safari hii miamba hiyo itakutana kwenye mchezo wa Raundi ya Tatu ya Kombe la FA huko uwanjani Emirates.

Wakati Arsenal ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya Man United kwa miaka ya hivi karibuni kwenye Ligi Kuu England, lakini linapokuja suala la Kombe la FA mara ya mwisho miamba hiyo ilipokutana Januari 2019, Man United ilishinda.

Lakini, gumzo la mechi ya keshokutwa ni kuhusu kutumiwa kwa mpira tofauti kabisa.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alilalamikia mpira uliotumika kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la Ligi wakati chama lake lilipochapwa na Newcastle United mabao 2-0 uwanjani Emirates, Jumanne iliyopita sasa kipute hicho cha keshokutwa, kitakuwa na mpira tofauti kabisa.

Kampuni ya Mitre inayosambaza mipira inayotumika kwenye michuano ya Kombe la FA imefichua kwamba mechi hiyo itashuhudia mpira tofauti ambao ni maalumu kama heshima kwa timu ya ugenini, Man United ambayo ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo.

Mpira huo unaitwa Ultimax Pro Winners Ball. Kwenye mechi nyingine za raundi ya tatu za Kombe la FA zitatumia mpira tofauti kabisa na huo ambao utachezwa huko Emirates.

Arteta anatazamiwa kusema kitu juu ya mpira huo maalumu ambao ni maalumu kwa ajili ya Man United endapo kama utakuwa na matokeo hasi upande wake.

Akizungumza baada ya Arsenal kuchapwa 2-0 na Newcastle, Arteta alisema: “Tumepiga mipira mingi sana nje ya goli. Ile mipira ilikuwa inapepea sana, kuna vitu vingi tulikuwa hatuvifahamu vizuri kuhusu ule mpira. Lakini, ndiyo hivyo mechi imekwisha na hatuna tunachoweza kubadili, tunasubiri mechi ijayo.”

Kwenye michuano yote iliyocheza msimu huu, Arsenal imekuwa na usahihi wa mashuti yake kwa asilimia 53 kwenye Kombe la Ligi, 52 kwenye Ligi Kuu England na 58 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini, kuhusu malalamiko ya mpira, EFL ilimjibu haraka Arteta kupitia msemaji wao, aliposema: “Kama ilivyohitajika kwenye mchezo huu, mipira ya Puma imekuwa ikitumika kwenye Kombe la Ligi na michuano ya EFL kwa msimu wa 2021/22 na ilifanyiwa majaribio kwa kuzingatia vigezo vya ubora wa Fifa na kukidhi viwango. Na cha ziada kwenye Kombe la Ligi, mpira huohuo unaotumika huko umekuwa ukitumika kwenye ligi nyingine kubwa za Ulaya, ikiwamo Serie A na LaLiga na madaraja yetu matatu ya EFL. Klabu zote zimetumia mpira huo huo na hatukupata malalamiko yoyote katika mechi 88 zilizopita.”

Arsenal na Man United ndiyo timu mbili zilizofanikiwa zaidi kwenye Kombe la FA, ambapo Arsenal imeshinda taji hilo mara 14 na Man United mara 13. Katika rekodi za jumla, Arsenal na Man United zimekutana mara 71, Arsenal imeshinda 24 na Man United 31, huku miamba hiyo ikitoka sare mara 16.

Katika mechi hizo, yamefungwa mabao 184, ambapo Arsenal 83 na Man United 101, ambapo kwenye Uwanja wa Emirates, zimecheza mechi 36, Atsenal imeshinda 17, Man United 11 na sare nane, wakati zilipokutana uwanjani Old Trafford, kwenye mechi 35, Arsenal imeshinda saba na Man United 20, huku mechi nane zilimalizika kwa sane.

Kwenye mechi za Ligi Kuu Englane, timu hizo zimekutana mara 59, Arsenal imeshinda 21, Man United 23 na sare 15, huku kwenye Kombe la Ligi imekutana mara moja na Man United ilishinda mechi hiyo, wakati kwenye Kombe la FA, timu hizo zimekutana mara sita, Arsenal imeshinda moja, Man United nne na sare moja.