Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mdau wa soka Nigeria awaonya viongozi NFF ishu ya Chelle

MDAU Pict

Muktasari:

  • Chelle, ambaye kwa sasa anapokea mshahara wa dola za Marekani 50,000 (Sh130 milioni) kwa mwezi, amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa. 

MWENYEKITI wa zamani wa Shirikisho la Soka la Jimbo la Gombe, Ahmed Shuaibu Gara-Gombe, ameuonya uongozi wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) kuhusu mchakato wa kusaini mkataba mpya na Kocha Mkuu wa Super Eagles, Eric Chelle.

Chelle, ambaye kwa sasa anapokea mshahara wa dola za Marekani 50,000 (Sh130 milioni) kwa mwezi, amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa. 

Mwishoni mwa wiki iliyopita, taarifa zilieleza kuwa, kocha huyo ameweka masharti 19 ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa la mshahara hadi dola 130,000 (Sh338 milioni), kupitia mkataba mpya anaotarajia kusaini.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Gara-Gombe amesema kwamba, kumpa Chelle mkataba mpya itakuwa ni kosa kwa soka la Nigeria. Aidha, amekosoa madai hayo ya kocha huyo akisema ni jaribio la kutumia nafasi yake kutokana na umaarufu alioupata kupitia Super Eagles.

“Sioni kama ni sawa,” Gara-Gombe amesema katika mahojiano na Gazeti la The Guardian.

Ameongeza: “Chelle alikuja Nigeria ili kuongeza wasifu wake. Super Eagles ni kubwa mno kwake. Anataka kututumia shinikizo baada ya Super Eagles kumweka katika jukwaa la kimataifa. Kwa wachezaji waliopo Nigeria, hata sisi tungekuwa tunamlazimisha kocha kama Eric Chelle kulipa ‘ada ya heshima’ kwetu.”

Gara-Gombe pia amepuuzia madai ya uhusiano kati ya Chelle na Olympique Marseille akisema ni hadithi ya kubuni, huku akisisitiza kwamba masharti ya kocha huyo yanaonekana kuwa hayana msingi.

“Akitaka kuondoka, aende. Sijawahi kuona mchango wa dhahiri kutoka kwake katika Super Eagles. Ikiwa tutamchagua tena Chelle kwa masharti haya, Nigeria itajutia,” ameongeza. 

Mbali na hitaji la mshahara wa mwezi wa dola 130,000 (Sh338 milioni), kiasi ambacho kinajumuisha pia malipo kwa kikosi chake cha kiufundi na msaidizi wake binafsi.

Chelle raia wa Mali, pia amesisitiza kuwa hatakubali kuingiliwa katika kazi zake, hasa kuhusiana na uongozi na usimamizi wa maendeleo ya timu za vijana za taifa.

Masharti haya yanajumuisha mahitaji mbalimbali ya kifedha na kiutawala, ikiwemo utoaji wa gari binafsi lenye dereva na ulinzi, makazi yenye usalama wa hali ya juu, huduma ya umeme isiyotetereka saa 24, ofisi yenye vifaa vya kisasa vya uchambuzi, huduma za intaneti, tiketi za ndege kwa familia yake, vifaa vya mazoezi, na uhuru kamili wa kuchagua mechi za kirafiki za kimataifa.

Aidha, Chelle anataka kuwepo kwa mipango madhubuti ya kambi za mazoezi, maendeleo ya vijana, na uwezo wa kusafiri kuangalia ligi ya ndani na wachezaji wa timu za taifa walioko nje ya nchi. Masharti mengine ni pamoja na kuhakikisha malipo ya mshahara yafanyika kabla au tarehe 30 ya kila mwezi, kuingizwa kwa msaidizi wake katika mpango wa bonasi na posho, na mikutano ya kila mwezi kati ya makocha wa timu zote za taifa.