Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eric Chelle aitega NFF, awasilisha masharti 19

CHELLE Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa masharti hayo ni ombi la mshahara wa mwezi wa dola 130,000 (Sh338 milioni), kiasi ambacho kinajumuisha pia malipo kwa kikosi chake cha kiufundi na msaidizi wake binafsi. 

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu Super Eagles, Eric Chelle, amewatia wasiwasi wapenzi wa soka wa nchi hiyo baada ya kuweka masharti 19 muhimu kabla ya kusaini mkataba mpya na Shirikisho la Soka Nigeria (NFF). 

Hali hiyo imetokea wakati huu ambapo mustakabali wa Chelle kuiongoza timu hiyo unaibuka kuwa na sintofahamu kubwa.

Miongoni mwa masharti hayo ni ombi la mshahara wa mwezi wa dola 130,000 (Sh338 milioni), kiasi ambacho kinajumuisha pia malipo kwa kikosi chake cha kiufundi na msaidizi wake binafsi. 

Chelle raia wa Mali, pia amesisitiza hatakubali kuingiliwa katika kazi zake, hasa kuhusiana na uongozi na usimamizi wa maendeleo ya timu za vijana za taifa.


Masharti haya yanajumuisha mahitaji mbalimbali ya kifedha na kiutawala, ikiwemo utoaji wa gari binafsi lenye dereva na ulinzi, makazi yenye usalama wa hali ya juu, huduma ya umeme isiyotetereka saa 24, ofisi yenye vifaa vya kisasa vya uchambuzi, huduma za intaneti, tiketi za ndege kwa familia yake, vifaa vya mazoezi, na uhuru kamili wa kuchagua mechi za kirafiki za kimataifa.

Aidha, Chelle anataka kuwepo kwa mipango madhubuti ya kambi za mazoezi, maendeleo ya vijana na uwezo wa kusafiri kuangalia ligi ya ndani na wachezaji wa timu za taifa walioko nje ya nchi. 

Masharti mengine ni pamoja na kuhakikisha malipo ya mshahara yafanyika kabla au tarehe 30 ya kila mwezi, kuingizwa kwa msaidizi wake katika mpango wa bonasi na posho na mikutano ya kila mwezi kati ya makocha wa timu zote za taifa.