Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

McTominey amtaka Mainoo aende fasta

MC Pict

Muktasari:

  • Mainoo, 20, amepoteza nafasi yake ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Ruben Amorim, ambapo kwa msimu huu amecheza dakika 138 tu kwenye Ligi Kuu England.

NAPLES, ITALIA: KIUNGO, Scott Mctominey ameitaka timu yake anayochezea Napoli kwenda kuvamia Manchester United kunasa huduma ya Kobbie Mainoo, ambaye hana furaha.

Mainoo, 20, amepoteza nafasi yake ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Ruben Amorim, ambapo kwa msimu huu amecheza dakika 138 tu kwenye Ligi Kuu England.

Kwa kutokuwapo kwenye michuano ya Ulaya na Man United kutupwa nje ya Kombe la Ligi mapema, Mainoo hapati nafasi ya kucheza na hilo limemweka kwenye wakati mgumu wa kupata nafasi ya kuwamo katika kikosi cha Thomas Tuchel cha Kombe la Dunia 2026 isipokuwa kama ataondoka Old Trafford wakati wa uhamisho wa Januari.

Kingine kinachomkwaza ni ishu ya mkataba wake, ambapo kwa sasa amekuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa mshahara mdogo na hakuna dalili za jambo hilo likapatiwa ufumbuzi siku za hivi karibuni.

Na ripoti zinafichua kwamba mchezaji mwenzake wa zamani waliyekuwa pamoja Old Trafford, McTominay, 28, amemtaka kocha wa Napoli, Antonio Conte kwenda kunasa huduma ya Mainoo ili akakipige Serie A.

McTominay alihamia Naples wakati wa dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana na alifunga mabao 12 katika msimu wake wa kwanza, Napoli iliposhinda taji la Serie A, huku yeye akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu na ligi na alishika namba 18 kwenye tuzo ya Ballon d’Or.

Chanzo cha habari kilibainisha: “Scott amekwenda kuonana na Conte na kumwambia amsajili Kobbie. Amemweleza kuhusu ubora wa mchezaji huyo na alivyoa hodari.”

McTominay anaamini Mainoo atakwenda kufiti vyema kwenye kikosi cha Napoli, ambayo kwenye dirisha lililopita ilimsajili Kevin de Bruyne kutoka Manchester City, ambaye kwa sasa atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji wa paja mwezi uliopita.