Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

McGinn atumia siku 10,225, kuandika rekodi mpya, Scotland ikianza vyema Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo ya leo ya kundi C, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Boston huko Foxborough, Massachusetts, Marekani, McGinn amefunga bao hilo katika ushindi wa 1-0, dhidi ya kikosi cha Haiti.

KIUNGO wa Scotland, John McGinn ameandika rekodi mpya ya kuifungia timu hiyo bao la kwanza katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia baada ya kutumia siku 10,225, tangu mara ya mwisho kwa kikosi hicho kiliposhiriki Ufaransa mwaka 1998.

Katika mechi hiyo ya leo ya kundi C, iliyopigwa kwenye Uwanja wa Boston huko Foxborough, Massachusetts, Marekani, McGinn amefunga bao hilo katika ushindi wa 1-0, dhidi ya kikosi cha Haiti.

Bao hilo la dakika ya 28, la kiungo huyo anayechezea Klabu ya Aston Villa ya Ligi Kuu ya England, ni la kwanza kwa Scotland katika fainali za Kombe la Dunia baada ya miaka 28, tangu mara ya mwisho, Craig Burley alipokifungia kikosi hicho mwaka 1998, huko Ufaransa.

Craig Burley ndiye aliyekuwa mchezaji wa mwisho kuifungia Scotland bao katika fainali za Kombe la Dunia, ambapo aliifungia timu hiyo katika sare ya 1-1, dhidi ya Norway, Juni 16, 1998.

Pia, bao hilo la McGinn limemfanya kushikilia rekodi ya mchezaji mkubwa zaidi kuifungia Scotland katika fainali za Kombe la Dunia, akiwa na miaka 31 na siku 238, akiipiku rekodi ya Kenny Dalglish aliyoiweka katika mechi ya timu hiyo dhidi ya New Zealand mwaka 1982, alipocheza na miaka 31 na siku 103.

Scotland inayojulikana kwa jina la utani la 'Tartan Army' kutokana na uhusiano mkubwa wa mashabiki wake, imerejea Kombe la Dunia 2026, kwa mara ya kwanza katika karne ya 21, baada ya miaka 28, tangu iliposhiriki mara ya mwisho mwaka 1998.

Timu hiyo imerejea Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28, ambapo mara ya mwisho kwa kikosi hicho kushiriki ilikuwa kwenye fainali za michuano hiyo ya mwaka 1998, iliyofanyika Ufaransa, huku ikiwa chini ya Kocha, Craig Brown.

Scotland inayofundishwa na Kocha, Steve Clarke ilifuzu michuano hiyo kwa staili ya aina yake baada ya kuifunga Denmark mabao 4-2, katika mechi kali ya kufuzu iliyopigwa kwenye Uwanja wa Hampden Park, Glasgow, Scotland, Novemba 18, 2025.

Timu hiyo iliingia katika michuano hii ikiwa na morali kubwa pia baada ya kufanya vizuri katika mechi mbili za kirafiki zilizochezwa siku za hivi karibuni, ikiifunga Curacao mabao 4-1, Mei 30, 2026, kisha kuichapa Bolivia 4-0, June 6, 2026.

Kwa upande wa Haiti maarufu 'Les Grenadiers' imefuzu Michuano ya Kombe la Dunia 2026, kwa mara ya kwanza katika historia yake baada ya miaka 52, tangu iliposhiriki mara ya mwisho mwaka 1974, kwenye fainali zilizofanyika Ujerumani Magharibi.

Haiti ilijihakikishia nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia baada ya kuifunga Nicaragua mabao 2-0, katika mechi ya mwisho ya kufuzu kutoka ukanda wa CONCACAF na kuongoza kundi C na pointi 11, ikishinda mechi tatu, sare mbili na kupoteza moja.

Katika kundi hilo la C, Haiti ilifuzu fainali za Kombe la Dunia mbele ya Honduras, Costa Rica na Nicaragua, ikiwa ni hatua muhimu ya historia, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona ikishindana tena dhidi ya mataifa makubwa duniani.

Ushindi huo kwa Scotland unaifanya kuongoza kundi C na pointi zake tatu, nyuma ya Brazil na Morocco zenye pointi moja kila mmoja baada ya sare ya kufungana bao 1-1, huku Haiti ikiburuza mkiani ikiwa