Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Knicks yatwaa ubingwa wa NBA baada ya miaka 53

Muktasari:

  • Huu ni ubingwa wa kwanza kwa Knicks tangu mwaka 1973, huku taji lao lingine likiwa lile la mwaka 1970.

SAN ANTONIO, MAREKANI: NEW  York Knicks imeandika historia mpya kwa kutwaa ubingwa wa NBA kwa mara ya kwanza baada ya miaka 53, kufuatia ushindi wa pointi 94-90 dhidi ya San Antonio Spurs katika mchezo wa fainali uliochezwa alfajiri ya leo, Jumapili mjini San Antonio.

Huu ni ubingwa wa kwanza kwa Knicks tangu mwaka 1973, huku taji lao lingine likiwa lile la mwaka 1970.

Mchezo huo wa fainali ya tano ulianza vizuri  kwa Spurs ambao walikuwa wakiongoza kwa pointi 16  katika robo ya pili kabla ya kibao kuwageukia.

Nyota wao, Victor Wembanyama alitumia urefu wake na uwezo wa kiufundi kuiongoza timu yake huku akirekodi vizuizi vitano (blocks) kabla ya mapumziko.

Knicks walionekana kuyumba mwanzoni mwa mchezo, wakifunga mitupuo matano kati ya 26 katika dakika 16 za kwanza, sawa na asilimia 19 ya mafanikio.

Aidha walifanya makosa tisa ya kupoteza mpira, jambo lililoisaidia Spurs kuweka tofauti  kubwa ya  pointi.

Hata hivyo, Knicks walijibu mapigo katikati ya robo ya pili wakiongozwa na nyota wao Jalen Brunson ambaye alimaliza kipindi cha kwanza akiwa amefunga pointi 16.

Mashabiki wa Knicks walipata matumaini baada ya timu yao kupunguza tofauti ya pointi hadi sita kufuatia mtupo wa  Mikal Bridges.

Dakika za mwisho za kipindi cha kwanza zilikuwa na ushindani huku Josh Hart akichangia pointi muhimu zilizoifanya Knicks kupunguza pengo hadi pointi tatu kabla ya Spurs kufunga mtupo wa  mwisho na kwenda mapumziko wakiwa mbele.

Kipindi cha pili kilianza kwa changamoto kwa Knicks baada ya Karl-Anthony Towns kupata kosa lake la nne, jambo lililomlazimu kukaa benchi kwa muda.

Spurs walitumia nafasi hiyo kurejesha uongozi wao hadi pointi 12.

Kulizuka pia utata baada ya Brunson kuanguka vibaya alipokuwa akitua baada ya mtupo wa pointi tatu huku yeye na kocha wake Mike Brown wakiamini kuwa Wembanyama alistahili kuadhibiwa kufuatia tukio hilo. Waamuzi hawakutoa adhabu yoyote.

Licha ya changamoto hizo, Knicks waliendelea kupambana na kupunguza tofauti ya pointi kabla ya robo ya mwisho kuanza Spurs wakiwa mbele kwa pointi 72-65.

Katika robo ya mwisho, Knicks walionyesha utofauti mkubwa  na hatumaye kugeuza kibao kwa   kuifunga Spurs kwa pointi 29-18 katika dakika 12 za mwisho za mchezo.

Kibao hicho kiliwapa ushindi wa pointi 94-90 na hatimaye kutwaa ubingwa wa NBA uliokuwa ukisubiriwa kwa zaidi ya nusu karne.