Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbrazili Oscar azua hofu Brazil

Muktasari:

  • Staa huyo wa zamani wa Chelsea aliishiwa nguvu wakati anafanya mazoezi ya kuendesha mashine inayofanana na baiskeli gym ndipo hapo alianza kujisikia vibaya.

SAO PAULO, BRAZIL: KIUNGO wa soka wa Kibrazili, Oscar amelazimika kuwahishwa hospitalini baada ya kuanguka ghafla akiwa mazoezini huko Sao Paulo.

Staa huyo wa zamani wa Chelsea aliishiwa nguvu wakati anafanya mazoezi ya kuendesha mashine inayofanana na baiskeli gym ndipo hapo alianza kujisikia vibaya.

Oscar, 34, alianguka chini na vyombo vya habari vya Brazil viliripoti alipoteza fahamu kwa kipindi cha dakika mbili.

Mchezaji huyo aliwahishwa katika hospitali ya Einstein Israelita ya huko Sao Paulo, Brazil kwa gari la wagonjwa ili kwenda kufanyiwa vipimo zaidi. Daktari mmoja alifanikiwa kumtuliza na kumrudisha Oscar kwenye ufahamu wake, lakini kilichogundulika ni kwamba ni tatizo la moyo.

Na klabu yake ilibainisha kwamba mchezaji huyo atabaki hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi wa afya yake ili kufahamu ukubwa wa tatizo.

Oscar alifanyiwa vipimo vya MRI ili kufahamu ukubwa wa tatizo lake. Na ripoti zaidi zilifichua kwamba kwa sasa Oscar anafikiria kustaafu soka kutokana na wasiwasi wa tatizo hilo.

Mkataba wake wa sasa kwenye kikosi cha Sao Paulo utafika tamati 2027, lakini sasa atalazimika kusitisha. Oscar aliichezea Chelsea kwa miaka mitano kabla ya kwenda kujiunga na Shanghai SIPG, ambayo kwa sasa inafahamika kama Shanghai Port alikoondoka Januari 2017.

Alicheza zaidi ya mechi 200 kwenye kikosi cha Chelsea kuanzia 2012 hadi 2017 na katika kipindi hicho alifunga mabao 38. Aliisaidia kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu England, huku akibeba pia Kombe la Ligi na Europa League.

Alitimkia China kwa uhamisho wa Pauni 60 milioni na kusaini mkataba wenye thamani ya Pauni 400,000 kwa wiki. Alicheza karibu miaka minane kwenye Chinese Super League kabla ya kuondoka kwenye ligi hiyo mwaka 2024. Oscar aliyevuna Pauni 175 milioni, alishinda mataji matatu huko Mashariki ya Mbali, akifunga mabao 77 na asisti 142. Baada ya kukaa siku 22 bila ya klabu, alisaini kuichezea Sao Paulo kwa mkataba wa miaka mitatu.