Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbio za ubingwa EPL, ukilala imekula kwako!

BACK Pict

Muktasari:

  • Lakini, Arsenal ya Kocha Mikel Arteta ipo mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya Man City ya Pep Guardiola. Hiyo ina maana, Man City ikishinda kiporo chake, itafanya pengo hilo la pointi kubaki kuwa mbili tu na kufanya vita ya ubingwa kuchukua sura mpya tofauti na hali ilivyokuwa wiki mbili au tatu zilizopita.

LONDON, ENGLAND: MSIMAMO wa Ligi Kuu England unavyosoma, Arsenal bado ipo kileleni kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili, Manchester City.

Lakini, Arsenal ya Kocha Mikel Arteta ipo mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya Man City ya Pep Guardiola. Hiyo ina maana, Man City ikishinda kiporo chake, itafanya pengo hilo la pointi kubaki kuwa mbili tu na kufanya vita ya ubingwa kuchukua sura mpya tofauti na hali ilivyokuwa wiki mbili au tatu zilizopita.

Utamu zaidi, mikikimikiki hiyo ya Ligi Kuu England itaendelea wikiendi hii na Man City itakuwa na nafasi ya kupunguza pengo hilo la pointi wakati itakapojimwaga uwanjani Etihad kukipiga na Newcastle United usiku wa Jumamosi. Patamu hapo.

Bila shaka, kocha Arteta atakuwa mbele ya runinga yake kutazama mechi hiyo, huku dua zake zitakuwa kwa Newcastle kuisimamisha Man City ili kupata ahueni katika mbio hizo za ubingwa kabla ya kuingia kwenye kasheshe lake Jumapili wakati atakapokabiliana na mahasimu wao wa London Kaskazini, Tottenham Hotspur ugenini.

Uzuri ni timu hizo zote mbili zilizopo kwenye mbio za ubingwa hakuna yenye mechi rahisi wikiendi hii. Man City ina kimeo cha Newcastle, ambao wamekuwa moto siku za karibuni, wakati Arsenal itakuwa na kasheshe la Spurs, iliyobadili kocha hivi karibuni.

Rekodi zinavyosoma, Man City na Newcastle zimekutana mara 51 kwenye Ligi Kuu England na 10 zilimalizika kwa sare, huku Man City ikishinda 32, mara 20 nyumbani na 12 ugenini, wakati Newcastle imeshinda tisa, nane nyumbani na moja tu ugenini. Lakini, mara ya mwisho timu hizo zilipokutana, Newcastle ilishinda 2-1 uwanjani St James' Park.

Kuhusu Arsenal na Spurs, zenyewe zimeshakutana mara 67 kwenye Ligi Kuu England na 24 zilitoka sare, huku Spurs ikishinda 15, mara 13 nyumbani na mbili tu ugenini, wakati Arsenal imeshinda 28, mara 20 nyumbani na nane ugenini. Mechi tano zilizopita baina yao, Arsenal imeshinda nne na sare moja.

Ukiweka kando vita hiyo ya kufukuzia ubingwa, kasheshe jingine kwenye Ligi Kuu England wikiendi hii ni kwenye Top Four. Aston Villa, Manchester United, Chelsea na Liverpool zipo kwenye vita kali na wikiendi hii kila moja, itarusha kete yake uwanjani.

Aston Villa kwenye nafasi ya tatu, itakuwa nyumbani kuwakabili Leeds United, ikiwa kwenye kampeni yake ya kujiimarisha kwenye nafasi hiyo, huku matokeo ya ushindi pia yatakuwa kitisho kwa Man City, kwasababu itakuwa imewafikia kwa pointi na hapo zitakuwa zimetofautiana mabao kabla ya Guardiola na chama lake hajawakabili Newcastle United usiku wa Jumamosi.

Chelsea kwenye nafasi ya tano itakuwa na nafasi ya kuishusha Man United kwenye nafasi ya nne wakati itakapokuwa nyumbani Stamford Bridge kukipiga na Burnley. The Blues itahitaji kushinda mechi hiyo ili kuipa presha Man United kwenye vuta nikuvute ya Top Four, huku kikosi hicho cha Old Trafford kinachonolewa na Michael Carrick kitakuwa uwanjani Jumatatu ugenini dhidi ya Everton.

Liverpool nayo kwenye namba sita itakuwa na nafasi ya kuifikia Man United kwa pointi, endapo itashinda ugenini dhidi ya Nottingham Forest huko City Ground, Jumapili. Jambo hilo litazidisha joto kwa Man United kuhakikisha inashinda dhidi ya Everton ili kuendelea kubaki kwenye Top Four.

Mechi nyingine zitakazopigwa Jumamosi ni Brentford itakuwa nyumbani kucheza na Brighton ikiwa moja ya mechi matata kabisa, huku West Ham ikiwa na kazi mbele ya Bournemouth, moja ya mechi zenye mvuto mkubwa.

Jumapili, mechi nyingine zitakazopigwa ni pamoja na ile ya Sunderland dhidi ya Fulham na Crystal Palace dhidi ya Wolves.

Jumatatu kutakuwa na mechi moja tu, Everton na Man United na rekodi zinasoma miamba hiyo imekutana mara 67 kwenye Ligi Kuu England na 14 zilimalizika kwa sare, huku Everton ikishinda 11, nane nyumbani na tatu ugenini, wakati Man United imeshinda 42, mara 23 nyumbani na 19 ugenini.

Mechi tano za mwisho, Man United imeshinda tatu, sare moja huku Everton ikishinda moja, ambayo ndiyo iliyokuwa ya mwisho wawili hao walipokutana Old Trafford.