Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbio za ubingwa EPL, Gary Neville aipa mbinu mpya Arsenal

UBINGWA Pict

Muktasari:

  • Neville ametoa kauli hiyo baada ya Arsenal kushinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Tottenham Hotspur jana Jumapili, Februari, 22, 2026, ushindi uliowawezesha kurekebisha nafasi yao na kuongoza msimamo wa EPL kwa tofauti ya pointi tano mbele ya Man City. Hata hivyo, timu ya Mikel Arteta imeshacheza mechi moja zaidi kuliko Man City.

Beki na nahodha wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, amesisitiza kuwa Arsenal lazima waibuke na ushindi dhidi ya Manchester City katika Uwanja wa Etihad iwapo wanataka kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu.

Neville ametoa kauli hiyo baada ya Arsenal kushinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Tottenham Hotspur jana Jumapili, Februari, 22, 2026, ushindi uliowawezesha kurekebisha nafasi yao na kuongoza msimamo wa EPL kwa tofauti ya pointi tano mbele ya Man City. Hata hivyo, timu ya Mikel Arteta imeshacheza mechi moja zaidi kuliko Man City.

Arsenal inatarajia kukutana na Manchester City katika fainali ya Kombe la Carabao Machi 22, 2026 kabla ya kutifuana ndani ya Ligi Kuu wa England, Aprili 18, 2026.

Akizungumza kupitia Sky Sports, Neville amesema: “Nimekuwa nikifikiria kwa muda mrefu Arsenal wanapokuwa wakipigania taji hili, lazima waende na kushinda Etihad. Hiyo ndiyo njia pekee halisi.

“Fainali ya Carabao Cup (Machi 22, 2026) ni fursa ya kutuma ujumbe, kwa sababu unacheza moja kwa moja dhidi yao, lakini kile unachoweza kufanya kweli ni kwenda na kuwapiga kwenye uwanja wao wenyewe.”

Ushauri wa Neville unasisitiza kuwa Arsenal itahitaji nguvu na mkakati thabiti ili kudhibiti ushindani kutoka kwa mabingwa wa Ligi Kuu, huku mashabiki wakitarajia pambano la ushindani mkubwa katika mechi zijazo.