Mbappe aweka rekodi mbovu

PARIS, UFARANSA. NYOTA wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe amekosa penalti mbili kwenye mechi ya Ligue 1 dhidi ya Montpellier na kuweka rekodi mbovu akiwa na klabu hiyo.
Kipa wa Montpellier alikuwa shujaa wa mchezo kwasababu alipangua penalti mbili zilizopigwa na Mbappe hata hivyo staa huyo akatolewa nje kutokana na majeraha.

Hata hivyo licha Mbappe kutolewa nje kutokana na majeraha PSG ikaibuka na ushindi wa mabao 3-1 yaliyowekwa kimiani na Fabian Ruiz dhidi ya 55, Lionel Messi akipachika bao dakika ya 72, Warren Zaire-Emery akishindilia msumari wa mwisho dakika ya 90, bao la Montpellier lilifungwa na Arnaud Nordin dakika ya 89.

Mbappe na Neymar walikuwa katika mzozo wa kugombea majukumu ya upigaji wa penalti kwenye timu, hata hivyo Mfaransa huyo ndio akapewa majukumu hayo lakini usiku wa kuamkia alikuwa na bahati mbaya.

Neymar aliukosa mchezo huo dhidi ya Montpellier kutokana na majeraha, sasa Messi atapewa majukumu ya upigaji wa penalti kipindi hichi ambacho Mbappe yupo nje baada ya kuumia.
Kocha wa PSG, Christophe Galtier alipata hofu baada ya Mbappe kufanyiwa mabadiliko mapema baada ya kuumia licha ya kukosa penalti mbili.

Baada ya mchezo huo dhidi ya Montpellier, PSG inajiandaa kucheza mechi yao nyingine ya ligi dhidi  Toulouse kesho bila ya mastaa wao Mbapoe na Neymar.