Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe avunja rekodi Real Madrid

MBAPPE Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Real Madrid alifunga mara tatu katika kipute hicho dhidi ya Barcelona kwenye mikimikiki ya La Liga kilichofanyika Jumapili na hivyo kufikisha mabao 39 msimu huu.

MADRID, HISPANIA: SUPASTAA, Kylian Mbappe hat-trick yake aliyoifunga kwenye El Clasico imemfanya avunje rekodi iliyokuwa imedumu kwa miaka 33.

Fowadi huyo wa Real Madrid alifunga mara tatu katika kipute hicho dhidi ya Barcelona kwenye mikimikiki ya La Liga kilichofanyika Jumapili na hivyo kufikisha mabao 39 msimu huu.

Licha ya kwamba fowadi huyo Mfaransa timu anayochezea ya Real Madrid kumaliza mechi hiyo kwa kichapo cha 4-3, matokeo ambayo yanaifanya Barcelona kuweka pengo la pointi saba kileleni na bado kuna mechi tatu kabla ya msimu kumalizika, lakini Mbappe aliweka alama zake kwenye La Liga.

Mbappe alifunga bao lake la kwanza kwa mkwaju wa penalti dakika ya tano kabla ya kuongeza la pili dakika tisa baadaye.

Barcelona ilijibu mapigo baada ya kufunga mara nne kabla ya mapumziko.

Mabao mawili ya Raphinha, moja la Eric Garcia na jingine la Lamine Yamal yalitosha kuipa ushindi muhimu Barcelona katika kipute hicho kilichofanyika uwanjani Estadi Olimpic Lluis Companys.

Mbappe alifunga tena kwenye kupindi cha pili na hivyo kukamilisha hat-trick yake.

Hata hivyo, matokeo hayo yanaifanya Barca sasa kuhitaji ushindi mmoja tu kwenye mechi tatu zilizobaki ili kutangaza ubingwa. Barca mechi yao ijayofuata watakipiga na mahasimu wao Espanyol.

Lakini, Mbappe ameshavunja rekodi kwenye klabu ya Real Madrid kwa mabao yake mawili ya kwanza kabla ya kufunga la tatu. Na sasa staa huyo amefikisha mabao 39 katika mechi 52 za michuano yote aliyochezea timu hiyo tangu alipohama kutoka Paris Saint-Germain mwaka jana.

Hiyo ni idadi kubwa zaidi ya mabao kufungwa kwenye msimu wa kwanza na mchezaji wa Real Madrid, hivyo amevunja rekodi ya Ivan Zamorano aliyoweka msimu wa 1992/93.

Zamorano alifunga mabao 37 katika mechi 45 alipotua kwenye timu hiyo akitokea Sevilla zaidi ya miongo mitatu iliyopita.

Mbappe pia amepiku rekodi ya mabao ya Cristiano Ronaldo aliyofunga kwenye mwaka wake wa kwanza Hispania. Staa huyo wa Ureno alifunga mabao 33 baada ya uhamisho wake akitokea Manchester United mwaka 2009.

Real Madrid imebakiza mechi tatu kwenye La Liga na itacheza pia Kombe la Dunia la Klabu.

Kwa sasa, Mbappe ndiye kinara wa mabao La Liga, akifikisha 26, huku akichuana na Robert Lewandowski kwenye mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu cha La Liga (Pichichi).

Mchezaji wa mwisho wa Real Madrid kuwa kinara wa mabao alikuwa Karim Benzema, alipofunga mara 27 katika msimu wa 2021/22.

Mechi zilizobaki itakipiga na Mallorca na Real Sociedad nyumbani na ugenini watakipiga na Sevilla.