Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe amkataa Mo Salah

MBAPPE Pict

Muktasari:

  • Ousmane Dembele yuko miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa baada ya kufunga mabao 33 na kusaidia Paris Saint-Germain kutwaa taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya, pia chipukizi wa Barcelona, Lamine Yamal, naye ni miongoni mwa wanaotajwa kutokana na kiwango alichoonyesha msimu huu.

PARIS, UFARANSA: STAA wa Real Madrid, Kylian Mbappe anaamini Mohamed Salah si miongoni mwa wachezaji wanaoweza kusumbua katika tuzo za Ballon d'Or ya mwaka huu na amemtaja ni mchezaji gani anampa nafasi ya kuchukua.

Ousmane Dembele yuko miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa baada ya kufunga mabao 33 na kusaidia Paris Saint-Germain kutwaa taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya, pia chipukizi wa Barcelona, Lamine Yamal, naye ni miongoni mwa wanaotajwa kutokana na kiwango alichoonyesha msimu huu.

Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, pia ametajwa kwenye mazungumzo hayo baada ya kuwa na msimu wa kuvutia akiiwezesha Liverpool kutwaa taji la Ligi Kuu England.

Hata hivyo, Mbappe hajamtaja kabisa Mmisri huyo alipoulizwa kuhusu chaguo lake kwa sasa kwenye tuzo hizo, ingawa alitoa tahadhari anaweza kubadili mawazo yake.

Akizungumza na tovuti ya RMC Sport, Mbappe alisema: "Dembele? Ndiyo. Sidhani hata kama kuna haja ya kutoa maelezo? Tunazungumza kuhusu Yamal na Dembele, mimi namchagua Dembele. Ni wazi kabisa!"

"Mambo hubadilika haraka sana, kama ilivyokuwa kwa washindi wa tuzo zilizopita. Kulikuwa na wachezaji ambao hatukuwa tunawazungumzia lakini walishinda. Ni Septemba? Mambo mengi yatafanyika kati ya sasa na wakati huo, lakini kwa sasa tunazungumzia kuhusu Ousmane na Lamine. Ndiyo maana nimejibu hivyo."

Mshindi wa Ballon d'Or mara tano, Cristiano Ronaldo, pia hivi karibuni alitoa maoni yake kuhusu tuzo hiyo, hasa akimzungumzia Lamine Yamal. Anaamini ni mapema kidogo kumwekea shinikizo kubwa kinda huyo, lakini anakubaliana staa huyo wa Barcelona anastahili kuwemo kwenye orodha.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na timu ya taifa ya Ureno, Ronaldo alisema: "Lamine Yamal anafanya vizuri sana, anatumia vyema kipaji chake. Lakini sasa aachwe akue, tusimweke chini ya presha kubwa. Aachwe awe yeye na akue kwa utaratibu."

Aliongeza: "Tuzo binafsi zimepoteza uhalali kiasi; siwezi kusema nani anapaswa kushinda. Kwa maoni yangu, anayeng’ara na kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya anastahili."

"Siamini sana katika tuzo binafsi kwa sababu najua yanayoendelea nyuma ya pazia. Lamine anaweza kushinda, kama Dembele au Vitinha, au wachezaji wengine wanaochipukia... Lakini tuzo binafsi si muhimu sana."

Ballon d'Or ya mwaka 2025 itatolewa Septemba katika hafla ya kifahari jijini Paris, huku wanaowania wakitarajiwa kuthibitishwa mwezi mmoja kabla. Kiungo wa Manchester City, Rodri, ndiye mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka uliopita.