Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe aishika pabaya PSG, adai Pauni 200 milioni

SES 01

Muktasari:

  • Mbappe aliondoka kwenye kikosi cha Ufaransa kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja, ambapo mechi yake ya mwisho kucheza ni ile aliyofunga mara mbili kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Ukraine.

PARIS, UFARANSA: SUPASTAA straika, Kylian Mbappe anahitaji alipwe zaidi ya Pauni 200 milioni kutoka Paris Saint-Germain huku sakata hilo likifikishwa mahakamani.

Mbappe aliondoka Parc des Princes kwenda kujiunga na Real Madrid wakati mkataba wake ulipofika ukomo Juni 2024. Jambo hilo liliifanya PSG kukosa ada ya uhamisho wa mchezaji huyo, kitu kilichomfanya mmiliki Nasser Al-Khelaifi kuchukia.

Lakini, gazeti la Ufaransa la Le Parisien limeripoti kwamba Mbappe anataka alipwe Pauni 211 milioni kutokana na kutokubaliana mambo fulani katika mchakato huo wa uhamisho wake.

Mbappe anawashutumu waajiri wake wa zamani kushindwa kufanya mkataba wake maalumu kuwa wa kudumu, huku wakishindwa kumlipa karibu Pauni 50 milioni ya mishahara yake na bonasi.

MBAP 01

Lakini, PSG imemjibu Mbappe juu ya matakwa yake ya kulipwa Pauni 158 milioni ikidai ilifanya hivyo baada ya mchezaji huyo kuahidi asingeondoka kama mchezaji huru kwenye timu.

PSG ilisema ilipokea ofa ya zaidi ya Pauni 260 milioni kutoka kwenye klabu moja ya Saudi Pro League miezi 12 kabla ya staa huyo wa zamani wa Monaco kuondoka bure na alikataa uhamisho huo wa kwenda Saudi Arabia.

Mbappe baadaye aligomea kuongeza mkataba mpya na kuifanya PSG kutokuwa na nguvu yoyote ya kumzuia asiende kujiunga na Real Madrid wakati mkataba wake ulipofika mwisho. Mbappe aliishutumu PSG pia ilitumia nguvu kumsainisha mkataba wenye masharti mapya badala ya kumwaacha amalizie ule wa awali.

MBAP 02

Mbappe alifunga mabao 256 katika mechi 308 alizochezea PSG. Aliasisti pia mara 110 huku akinyakua taji la Ligue 1 mara sita katika kipindi chake cha mataji mengi aliyobeba huko Parc des Princes.

Mbappe amefunga mara 18 katika mechi 16 alizochezea Real Madrid msimu huu, huku akishindwa kufunga kwenye mechi mbili tu za La Liga. Lakini, sasa ripoti za kuwa majeruhi zinatishia uwezekano wa kuwapo kwenye mechi ijayo ya La Liga dhidi ya Elche, Jumapili.

Mbappe aliondoka kwenye kikosi cha Ufaransa kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja, ambapo mechi yake ya mwisho kucheza ni ile aliyofunga mara mbili kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Ukraine.