Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe aibua hofu Madrid

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Les Bleus alifunga mara mbili kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Ukraine, Alhamisi iliyopita na kuisaidia timu yake kukamatia tiketi ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

MADRID, HISPANIA: SUPASTAA, Kylian Mbappe ameibua wasiwasi mkubwa huko Real Madrid baada ya kuondoka kwenye kambi ya Ufaransa kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya enka.

Fowadi huyo wa Les Bleus alifunga mara mbili kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Ukraine, Alhamisi iliyopita na kuisaidia timu yake kukamatia tiketi ya fainali za Kombe la Dunia 2026.

Na Mbappe alikuwa na matumaini ya kwenda kukabiliana na Azerbaijan, Jumapili kuendeleza moto wa timu yake wa kucheza bila ya kupoteza.

Lakini, mkali huyo hatakuwapo kwenye mechi hiyo kutokana na kuwa na maumivu kwenye enka ya mguu wake wa kulia, ambao umemfanya aondoke kambini mapema ili kujitibu.

Shirikisho la soka la Ufaransa (FFF) limethibitisha hilo na kusema Mbappe amerudi Madrid kwenda kupatiwa matibabu zaidi.

Kwenye ripoti hiyo imefichuka pia Eduardo Camavinga naye atarudi Madrid kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kina kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli, huku mchezaji Manu Kone akikabiliwa na adhabu.

Taarifa ya FFF ilibainisha: “Mastaa wa kimataifa wa Ufaransa Manu Kone, Eduardo Camavinga, na Kylian Mbappe wameondoka kambini kwenda kujiunga na klabu zao. Kikosi cha Ufaransa kitaenda Baku kukabiliana na Azerbaijan, Jumapili na Camavinga, Kone na Mbappe hawatakuwapo kwenye msafara.

“Kone alionyeshwa kadi ya njano dhidi ya Ukraine na hivyo amekumbana na adhabu. Cama anasumbuliwa na maumivu ya misuli, hasa kwenye paja lake la mguu wa kushoto. Mbappe anasumbuliwa na maumivu ya enka ya mguu wa kulia, atahitaji uchunguzi.”