Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayweather, Pacquiao kuna utata

PAMBANO Pict

Muktasari:

  • Miaka tisa baada ya pambano lake la mwisho la kiushindani dhidi ya bingwa wa zamani wa UFC, Conor McGregor, Mayweather anatarajiwa kurejea tena ulingoni mwaka huu kupambania rekodi yake ya kutopoteza pambano la kimashindano.

LAS VEGAS, MAREKANI: PAMBANO kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao bado linatarajiwa kuwepo kama lilivyopangwa licha ya taarifa Mayweather amevunja mkataba wa pambano hilo.

Miaka tisa baada ya pambano lake la mwisho la kiushindani dhidi ya bingwa wa zamani wa UFC, Conor McGregor, Mayweather anatarajiwa kurejea tena ulingoni mwaka huu kupambania rekodi yake ya kutopoteza pambano la kimashindano.

Tangu pambano la McGregor, Mayweather, 49 amekuwa akishiriki mapambano yasiyo ya kiushindani rasmi ambayo hayaathiri rekodi yake.

Hata hivyo, Septemba 19 mwaka huu, anatarajiwa kupanda ulingoni kumkabili mpinzani wake mkubwa, Manny Pacquiao, katika pambano rasmi la ushindani.

Lakini utata umeibuka baada ya Mayweather kudai, pambano hilo ni la maonyesho na halitokuwa katika rekodi zake za kitaaluma.

Akizungumza na mashabiki jijini Las Vegas, bondia huyo amesema: "Hatujui mahali pambano litakapofanyika. The Sphere ni moja ya sehemu zilizotajwa. Na hili si pambano rasmi, ni la kirafiki tu."

Kauli hiyo imesababisha mjadala mkubwa, huku Mkurugenzi Mtendaji wa MannyPacquiao Promotions, Jas Mathur, akidai Mayweather amevunja mkataba.

Akizungumza na ESPN, Mathur amesema: “Kwa sasa pambano bado lipo. Halijavunjwa na Mayweather amesaini kupigana pambano la kiushindani na siyo kirafiki au maonyesho kama anavyodai. Kauli zake zinaonyesha amekiuka mkataba. Tumeendelea kuwasiliana na timu yake, lakini wanasisitiza kubadili pambano liwe la kirafiki, jambo ambalo linakwenda kinyume na makubaliano."

Mathur pia alifichua Mayweather tayari amelipwa fedha nyingi kama sehemu ya malipo ya awali ya pambano hilo.

“Mayweather alisaini mikataba mitatu tofauti katika tarehe tofauti Oktoba 24, Novemba 6, na Desemba 14 na alipokea malipo kwa kila mkataba. Kama anaogopa kupambana na Manny na hataki kuweka rekodi yake hatarini, hakupaswa kusaini mikataba hiyo. Anatakiwa kutoka wazi na kusema ukweli  kwa sababu Manny haogopi.”

Licha ya mvutano huo wa kimkataba, dalili zinaonyesha kuwa pambano hilo kubwa bado linaweza kufanyika kama lilivyopangwa, ingawa pande zote mbili zinatakiwa kukubaliana kwanza.