Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mavitu ya Sterling huko Arsenal balaa

Muktasari:

  • Winga huyo aliyechezea England mara 82 aliwatesa kwa chenga kali wachezaji watatu mazoezini kwenye kikosi hicho cha Kocha Mikel Arteta huko London Colney wiki iliyoisha.

LONDON, ENGLAND: RAHEEM Sterling amewaonyesha Chelsea kile watakachokikosa msimu huu baada ya kuonyesha mavitu ya maana kwenye mazoezi ya timu yake mpya ya Arsenal.

Winga huyo aliyechezea England mara 82 aliwatesa kwa chenga kali wachezaji watatu mazoezini kwenye kikosi hicho cha Kocha Mikel Arteta huko London Colney wiki iliyoisha.

Sterling, 29, alijiunga na Arsenal kwa mkopo wa msimu mzima katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili na hakutaka kuchukua muda mrefu kuonyesha kile ambacho miguu yake inaweza kufanya uwanjani.

Staa huyo wa zamani wa Manchester City aliwalamba chenga wachezaji watatu wa Arsenal mazoezini, akiwamo kiungo mmoja mgumu alipokuwa akionyesha maujuzi yake Alhamisi iliyopita.

Jorginho na makinda wawili Harrison Dudziak na Ife Ibrahim walibaki wakishangaa tu, wakati Sterling alipopita na mpira katikati yao na kuenda zake, huku kila mmoja akipigwa chenga ya mwili na kubaki hoi.

Leandro Trossard, ambaye alitemwa kikosi cha Ubelgiji kilichocheza Nations League, alijaribu kuja kumzuia Sterling, lakini naye alikuwa ameshachelewa, Mwingereza huyo alikuwa ameshatoka eneo hilo.

Katika video nyingine ya mazoezini, mshindi huyo mara nne wa Ligi Kuu England alionekana akipiga mashuti na kufunga na kuwafanya mashabiki wa Arsenal kutaka ligi irejee haraka.

Hata kwenye pasi zake za kugonga moja moja, zilikuwa moto na kumfanya shabiki mmoja akiandika kwenye mitandao ya kijamii: “Hebu ona huruma, Raheem.”

Mwingine aliandika kwenye X: “Mabeki watakuwa kwenye usingizi mnono wakati Sterling akiwamaliza.” Shabiki wa tatu alisema: “Nimefurahi sana kumwona akicheza.”

Na shabiki wa nne aliongeza: “Raheem amewaka kwa sasa.”

Sterling aliondoka Chelsea baada ya kocha wa miamba hiyo, Enzo Maresca kumwambia hana nafasi kwenye kikosi chake kwa msimu huu.