Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauricio Pochettino afunguka hatma yake

POCHE Pict

Muktasari:

  • Pochettino, raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 54, anamaliza mkataba wake wa sasa na tayari amewekewa mezani ofa ya kuongeza kandarasi kwa miaka minne, ambayo ingemuweka madarakani hadi baada ya Kombe la Dunia la mwaka 2030.

LOS ANGELES, MAREKANI: KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Marekani, Mauricio Pochettino, amesema atachukua muda wa kupumzika baada ya kumalizika kwa kampeni ya Kombe la Dunia kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake.

Pochettino, raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 54, anamaliza mkataba wake wa sasa na tayari amewekewa mezani ofa ya kuongeza kandarasi kwa miaka minne, ambayo ingemuweka madarakani hadi baada ya Kombe la Dunia la mwaka 2030.

Licha ya kupewa nafasi hiyo, kocha huyo amesema bado hajafikia uamuzi wa kuendelea kuinoa Marekani.

"Tulikuwa na mazungumzo na Shirikisho la Soka la Marekani. Kwa sasa nafikiri ni wakati wa kupumzika kidogo, kisha tutakaa chini kujadili na kuona uamuzi utakaochukuliwa na shirikisho pamoja na sisi," amesema Pochettino.

Aliongeza: "Nimefurahia sana uhusiano tulioujenga na shirikisho, lakini huu si wakati sahihi wa kuzungumzia mustakabali wangu."

Kauli hiyo imekuja dakika chache baada ya Marekani kutolewa kwenye Kombe la Dunia kufuatia kipigo kizito cha mabao 4-1 dhidi ya Ubelgiji.

Katika mchezo huo, Charles De Ketelaere, aliifungia Ubelgiji mabao mawili, huku Malik Tillman akiifungia Marekani bao pekee kupitia mpira wa adhabu uliobadili mwelekeo. Makosa ya kipa Matt Freese yalichangia Hans Vanaken kufunga bao la tatu kabla ya Romelu Lukaku kuhitimisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne katika dakika za nyongeza.

Matokeo hayo yalihitimisha safari ya Marekani kwenye Kombe la Dunia ililokuwa likiandaa kwa maumivu makubwa mbele ya mashabiki wake.

Baada ya mchezo, beki nyota wa Marekani Chris Richards alimpongeza Pochettino kwa mchango wake mkubwa ndani ya kikosi.

"Amekuwa na ushawishi mkubwa kwetu, hasa katika miezi 18 iliyopita. Kila mtu ameona namna timu ilivyokua. Si kila kitu kilikuwa kamili, lakini maendeleo yamekuwa makubwa," amesema Richards.

Aliongeza: "Ameisaidia sana timu hii, amesaidia maendeleo ya soka la taifa letu na hata mimi binafsi. Nina matumaini ataongeza mkataba wake. Kama ataendelea, naamini katika Kombe la Dunia lijalo tutafika mbali zaidi."

Pochettino ndiye kocha anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya soka la Marekani, akivuna dola milioni sita kwa mwaka, lakini sasa macho yote yameelekezwa kwenye uamuzi wake kuhusu kubaki au kuhitimisha safari yake na timu hiyo baada ya kushindwa kutimiza ndoto ya kufanya vizuri katika Kombe la Dunia.