Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastraika waliofunika kibabe msimu wa 2020/21

LONDON, ENGLAND. STRAIKA, Luis Suarez amekuwa na msaada mkubwa kwelikweli Atletico Madrid kwa msimu huu baada ya kuisaidia miamba hiyo ya Madrid kubeba ubingwa wa La Liga. Suarez, ambaye aliondoshwa kwa masimango Barcelona, amefunga mabao 21 kwenye La Liga msimu huu na kuisaidia Atletico kuvuna pointi 21 katika kampeni yao ya kunyakua ubingwa wa msimu huu.

Jambo hilo linamfanya supastaa huyo wa kimataifa wa Uruguay kuwa mmoja wa washambuliaji wa kati matata kabisa waliotamba kwenye ligi za msimu huu na kusaidia timu kwa namna fulani. Hakuna ubishi, kwa timu ambayo ina shida ya straika kama itaingia sokoni na kunasa moja ya huduma za wakali hawa basi watakuwa wamepiga bonge la bao!


11. Wissam Ben Yedder (AS Monaco)

Kwenye orodha ya washambuliaji wa kati waliowasha moto kibao kwa ligi za msimu huu, Wissam Ben Yedder ni mmoja wao kutokana na kile alichokifanya AS Monaco kwenye mikikimikiki ya Ligue 1. Staa huyo ametupia wavuni mabao 20 katika mechi 36 alizocheza kwenye ligi hiyo huku akiwa na mchango mkubwa kwa timu yake uwanjani.

10. Andre Silva (Eintracht Frankfurt)

Andre Silva ametua kwenye Bundesliga na kuikamatia kibabe msimu huu wa 2020/21, ambapo alifunga mabao 28 katika mechi 32. Umri wake ndio kwanza miaka 25 na kinachoonekana ni suala la muda tu kabla ya kukamatia dili moto kabisa la kwenda kujiunga na klabu kubwa Ulaya, huku vigogo kibao vya England zikimsaka kimyakimya.


9. Luis Muriel (Atalanta)

Staa Luis Muriel amekuwa kwenye kiwango bora kabisa huko Italia msimu huu na hakika ameonyesha thamani yake kwenye kikosi cha Atalanta. Straika huyo wa kimataifa wa Colombia, amefunga mabao 22 kwenye mikikimikiki ya Serie A ikiwa ni wastani wa bao moja katika kila dakika 63 alizokuwa uwanjani, kitu ambacho kimeonyesha ubora.


8. Gerard Moreno (Villarreal)

Villarreal imefunga mabao 60 kwenye La Liga msimu huu, huku straika Gerard Moreno akuhusika kwenye asilimia 50 ya mabao hayo, akifunga mara 23 na kuasisti mara saba. Hayo ndo makali ya straika huyo matata kabisa wa Kihispaniaola, ambaye anastahili nafasi kwenye fowadi ya La Roja kwenye fainali zijazo za Euro 2020.


7. Karim Benzema (Real Madrid)

Karim Benzema amethibitisha kuwa yeye ni kama mvinyo. Kwa kadri unavyozidi kuwa na miaka mingi, ndicho unachoweza kusema kuhusu straika huyo Mfaransa. Umri wake ni miaka 33, lakini hilo halijawa tatizo kabisa, akifunga mabao 30 kwenye michuano yote kwa msimu huu kitu ambacho kimeonyesha amestahili kuitwa Les Bleus.

6. Romelu Lukaku (Inter Milan)

Straika, Romelu Lukaku amewanyamazisha wale waliokuwa wakihoji uwezo wake baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa Inter Milan. Staa huyo Mbelgiji amekuwa sehemu muhimu ya ubingwa wa Serie A kwa Inter msimu huu, akifunga mabao 24 kwenye ligi, huku akionyesha kiwango bora kabisa ndani ya uwanja. Timu sasa zinamsaka.

5. Luis Suarez (Atletico Madrid)

Uamuzi wa Barcelona kumuuza Luis Suarez umewatokea puani, wamefanya kosa kubwa sana. Straika huyo mwenye umri wa miaka 34 ndiye aliyeamua ubingwa wa La Liga msimu huu, akiipa taji hilo chama lake jipya la Atletico Madrid. Mabao yake 21 aliyofunga yaliisaidia Atletico kuvuna pointi 21 na hivyo kunyakua taji kibabe kabisa.


4. Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain)

Supastaa, Kylian Mbappe alionyesha kiwango bora kabisa alipochezeshwa nafasi ya mshambuliaji wa kati kwenye kikosi cha PSG msimu huu 2020/21, aliipiga hat-trick Barcelona tena kwao Nou Camp, kisha akaichapa mbili Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Amefunga mabao 27 katika mechi 31 alizocheza kwenye Ligue 1.


3. Erling Haaland (Dortmund)

Kama kuna jina la mshambuliaji wa kati ambalo linasakwa karibu na kila timu kigogo Ulaya basi ni la Erling Haaland. Staa huyo wa Norway, ameonyesha kiwango bora kabisa msimu huu. Amemaliza msimu kwa kufunga mabao 41 katika michuano yote, idadi ya mabao ambayo haijawahi kufikiwa na mchezaji mwenye umri wa miaka 20.


2. Harry Kane (Tottenham Hotspur)

Harry Kane amethibitisha msimu huu kwamba ni mshambuliaji wa kati aliyekamilika. Straika huyo, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya England, ameibeba Spurs akifunga mabao 23 yaliyomfanya ashinde Kiatu cha Dhahabu kwenye ligi na kuasisti mara 14, ambapo alibeba tuzo pia. Ametangaza anatafuta timu mpya msimu ujao.


1. Robert Lewandowski (Bayern Munich)

Nani anabisha? Lewandowski ndiye straika bora kabisa duniani kwa sasa. Supastaa huyo wa Poland ameweka rekodi ya kibabe kabisa kwenye kikosi cha Bayern Munich, akifunga mabao 41 ndani ya msimu mmoja tu wa ligi, huku akiwa amecheza mechi 29. Ndiye mshambuliaji wa kati anayepewa nafasi kubwa ya kushinda Ballon d’Or 2021.