Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Waafrika LaLiga kuwania tuzo Afrika

LA LIGA Pict

Muktasari:

  • Tuzo hiyo ambayo sasa inatolewa kwa mara ya tano, inaendelea kuonyesha mchango mkubwa wa wachezaji wa Kiafrika katika LaLiga pamoja na kuimarisha ushawishi wao katika soka la Ulaya.

MADRID, HISPANIA: LIGI Kuu Hispania (LaLiga) imetangaza orodha ya wachezaji walioteuliwa kuwania tuzo ya Sporty LaLiga MVP 2025/26, inayotambua mchezaji bora kutoka Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara anayeshiriki ligi hiyo msimu huu.

Tuzo hiyo ambayo sasa inatolewa kwa mara ya tano, inaendelea kuonyesha mchango mkubwa wa wachezaji wa Kiafrika katika LaLiga pamoja na kuimarisha ushawishi wao katika soka la Ulaya.

Mshindi wa mwaka huu ataungana na orodha ya nyota waliowahi kushinda tuzo hiyo akiwemo mshindi mara mbili Inaki Williams pamoja na Samuel Chukwueze na Yassine Bounou.


UPIGAJI KURA

Upigaji kura ulianza juzi, na mashabiki wanaweza kupiga kura hadi Jumapili, Mei 10, 2026, ambapo mshindi ataamuliwa kupitia kura za mashabiki kutoka Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara pamoja na jopo la wataalamu likijumuisha waandishi wa habari na wadau wa soka.

Mshindi atatangazwa katika hafla maalumu itakayofanyika Lagos, Nigeria, Mei 23, mwaka huu sambamba na wiki ya mwisho ya msimu wa LaLiga.

Tuzo hiyo inaandaliwa kwa ushirikiano na Sporty Group, kampuni ya burudani na teknolojia ya michezo Afrika, ikiwa na lengo la kuimarisha uhusiano kati ya soka la Hispania na Afrika.


WASIKIE WADAU

Mkurugenzi wa chapa wa Sporty Group, Miguel Puche, alisema tuzo hiyo inaonyesha mchango mkubwa wa wachezaji wa Afrika katika soka la Hispania na jinsi wanavyowaunganisha mashabiki duniani.

Kwa upande wake, Tresor Penku wa LaLiga Africa alisisitiza kuwa soka la Afrika limekuwa sehemu muhimu ya historia ya ligi hiyo na linaendelea kukua kila msimu.

Kwa kifupi tuzo hiyo si tu ya ushindani, bali pia ni ishara ya heshima kwa vipaji vya Kiafrika vinavyoendelea kung’ara Ulaya.