Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashindano ya WAFCON 2026 yapelekwa mwezi Julai

WAFCON Pict

Muktasari:

  • Awali, michuano hiyo ilipangwa kufanyika kuanzia Machi 17, 2026 hadi Aprili 3, 2026, lakini sasa itafanyika kuanzia Julai 25, 2026 hadi Agosti 16, 2026.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF), limetangaza kuahirishwa kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2026), uamuzi uliotolewa siku 12 zikisalia kabla ya kuanza kwa mashindano hayo nchini Morocco.

Awali, michuano hiyo ilipangwa kufanyika kuanzia Machi 17, 2026 hadi Aprili 3, 2026, lakini sasa itafanyika kuanzia Julai 25, 2026 hadi Agosti 16, 2026.

CAF imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya mazungumzo na serikali ya Morocco, FIFA, na wadau wengine ili kuhakikisha mafanikio ya mashindano hayo kutokana na changamoto ambazo hazikutarajiwa.

Hatua hiyo inamaliza sintofahamu ya kama Morocco ingeendelea kuwa mwenyeji, baada ya Afrika Kusini kuonyesha nia ya kutaka kuchukua nafasi hiyo kufuatia kusuasua kwa maandalizi ya awali.

Waziri wa Michezo wa Afrika Kusini, Gayton McKenzie, aliwahi kunukuliwa akisema nchi yake ilikuwa tayari kuandaa michuano hiyo iwapo Morocco isingeweza, akisisitiza kuwa soka la wanawake halipaswi kuchukuliwa kwa mzaha.

Makundi ya WAFCON 2026:
Licha ya mabadiliko ya tarehe, makundi ya timu 16 yalishapangwa kama ifuatavyo:

Kundi A (Rabat): Morocco (Wenyeji), Algeria, Senegal, na Kenya.

Kundi B (Rabat): Afrika Kusini, Ivory Coast, Burkina Faso, na Tanzania.

Kundi C (Casablanca): Nigeria (Mabingwa watetezi), Zambia, Misri, na Malawi.

Kundi D (Fes): Ghana, Cameroon, Mali, na Cape Verde.

UMUHIMU WA WAFCON 2026
Kufuzu Kombe la Dunia: Michuano hii ndiyo itakayotoa timu nne zitakazoiwakilisha Afrika katika Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA 2027 nchini Brazil.

Ongezeko la Zawadi: Rais wa CAF, Patrice Motsepe, ameahidi kuongeza kiwango cha zawadi kwa washindi, ambapo bingwa wa mwisho (Nigeria) alipewa dola milioni 1 (Sh2.6 bilioni).

Wageni wa Mashindano: Mataifa ya Malawi na Cape Verde yatashiriki kwa mara ya kwanza, ikionyesha kukua kwa soka la wanawake barani.

Kusogezwa huku kwa tarehe kumeleta changamoto ya mipango kwa timu zinazoshiriki, lakini kunatoa nafasi kwa mashindano hayo kufanyika mara baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia la Wanaume la 2026.