Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Martinelli afurahia ushindani Arsenal

MARTINELI Pict

Muktasari:

  • Martinelli, 24, amekuwa kwenye mashaka makubwa juu ya hatima yake kwenye kikosi cha Arsenal baada ya miamba hiyo inayonolewa na kocha Mikel Arteta kufanya usajili wa mawinga wengine, Noni Madueke na Eberechi Eze wanaokwenda kuleta ushindani mkali wa namba.

LONDON, ENGLAND: WINGA wa Arsenal, Gabriel Martinelli amesema tena kwa msisitizo kwamba anafurahia ushindani wa namba uliopo kwenye kikosi hicho na yupo tayari kwa mapambano licha ya kuwapo na taarifa za kwamba anafikiria mipango wa kuondoka Emirates.

Martinelli, 24, amekuwa kwenye mashaka makubwa juu ya hatima yake kwenye kikosi cha Arsenal baada ya miamba hiyo inayonolewa na kocha Mikel Arteta kufanya usajili wa mawinga wengine, Noni Madueke na Eberechi Eze wanaokwenda kuleta ushindani mkali wa namba.

Kulikuwa na ripoti kwamba Arsenal itakuwa tayari kupokea ofa ya kumuuza Mbrazili huyo, huku ikielezwa Pauni 60 milioni itatosha kabisa kwa staa huyo kung'oka Emirates.

Hata hivyo, timu nyingi zilimthaminisha Martinelli kuwa na thamani ya Pauni 40 milioni, licha ya Mbrazili huyo kujihakikishia nafasi ya kucheza kwenye wingi ya kushoto ya Arsenal, ambako msimu uliopita alikuwa akipewa nafasi sana Leandro Trossard.

Martinelli alifunga mabao 10 katika michuano yote msimu uliopita licha ya kucheza mechi 51 za klabu hiyo ya Arsenal. Pamoja na ushindani uliopo wa nafasi kwenye kikosi hicho, Martinelli yupo tayari kwa vita.

"Kwa kulinganisha na Arsenal, ni kama ilivyo kwenye timu ya taifa," alisema Martinelli alipokuwa kwenye majukumu ya kuitumikia Brazil kwenda mechi ya kimataifa.

"Kama utaniuliza kama ni jambo zuri kuwa na Vini au Rodrygo kwenye timu ya taifa, nitakwamba ndio. Kwa sababu watasaidia timu kubwba mataji. Na kama unataka kushinda, unahitaji wachezaji wenye viwango. Ni hivyo kama ilivyo Arsenal. Nafurahia ujio wa Eze na Madueke. Trossard naye anacheza upande wa kushoto. Nafurahi kuona wachezaji wenye viwango kwenye kikosi chetu. Tuna mechi nyingi sana kwa msimu. Vitu vingi hutokea, majeruhi na mengineyo.

"Hivyo, ni jambo zuri kwa klabu kusajili wachezaji mahiri kwenye ligi, tunaweza kushinda."