Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maresca afunguka majanga yake Chelsea

Muktasari:

  • Bosi huyo wa The Blues aliangusha dundo Jumamosi iliyopita alipodai amepita kwenye siku mbili mbaya sana tangu alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa miamba hiyo ya Stamford Bridge.

LONDON, ENGLAND: KOCHA Enzo Maresca amesema yupo na furaha kubwa huko Chelsea, lakini amegoma kupuuzia malumbano yake na mabosi kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge.

Bosi huyo wa The Blues aliangusha dundo Jumamosi iliyopita alipodai amepita kwenye siku mbili mbaya sana tangu alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa miamba hiyo ya Stamford Bridge.

Akizungumza kabla ya mechi ya robo fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Cardiff City usiku wa Jumanne, Maresca alipewa dakika 10 za kufafanua maelezo yake. Maresca alisema maofisa walimweleza kwa uwazi kabisa, hivyo hawezi kuomba radhi kwa chochote. Na alipoulizwa kama anafurahia maisha yake Stamford Bridge, Maresca alisema: “Kabisa, jibu ni ndiyo.”

Kocha huyo Mtaliano aliulizwa kuhusu hali ya sintofahamu kwenye klabu hiyo wakati wa ushindi dhidi ya Everton Jumamosi iliyopita na ulikuja baada ya kucheza mechi nne bila ya kupata ushindi.

Alipoulizwa alichokieleza ni kuhusu kushindwa kupata sapoti kutoka kwa wamiliki wa Chelsea, Maresca alisema: “Nishazungumza juu ya hilo, sitaki kuongeza vitu vingine. Nilishasema juu ya hilo na nadhani lilikuwa bayana.

“Naheshimu maoni yangu, lakini sitaki kuongeza kitu, akili yangu ipo kwenye mechi ya Cardiff na mpango wa kufika nusu fainali na itakuwa mara yangu ya tatu kufika hatua hiyo tangu nilipojiunga na klabu hii.”

Maresca alisema kiungo wake mshambuliaji Cole Palmer asingetumika kwenye mechi ya Cardiff City.