Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maresca afunguka ishu ya kipa wake

Muktasari:

  • Sanchez alitokea bila ya umakini mzuri kiasi cha kumpatia Erling Haaland  nafasi nzuri ya kuifungia bao la pili Man City katika ushindi wa 3-1, matokeo ambayo yaliwaweka mabingwa hao watetezi katika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya kufanya makosa yaliyochangia Chelsea kupoteza dhidi ya Manchester City wikiendi iliyopita, kipa wa miamba hiyo ya Stamford Bridge, Robert Sanchez huenda akakaa benchi kwa mechi zijazo, kwa mujibu wa kocha Enzo Maresca.

Sanchez alitokea bila ya umakini mzuri kiasi cha kumpatia Erling Haaland  nafasi nzuri ya kuifungia bao la pili Man City katika ushindi wa 3-1, matokeo ambayo yaliwaweka mabingwa hao watetezi katika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu England.

Tangu kuanza kwa msimu huu Sanchez amefanya makosa matano yaliyozaa mabao, na Maresca tayari ameshamweka nje katika mechi mbili dhidi ya Southampton na Ipswich ambapo alianza na  Filip Jorgensen ambaye anaweza kucheza katika mechi ijayo dhidi ya West Ham.

“Tunamwamini Robert na anafahamu kwamba anafanya makosa, tunaendelea kumwamini Robert, lakini bado tuna wiki nzima, tutaangalia kile atakachoonyesha mazoezini na kuamua hatma yake kwa michezo inayofuata.”

Maresca alikiri kabla ya mechi kwamba Sanchez “bado yuko mbali sana na mahali ninapotaka awe,” na inaonekana mustakabali wa staa huyu raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 27 uko hatarini.

“Robert anajua kabisa kwamba lazima afanye vizuri zaidi, anajua vyema. Kwa sasa hali iko hivyo.”

Kosa la Sanchez lilifunika mwanzo mgumu wa beki mpya wa kati wa Man City aliyenunuliwa kwa pauni 33 milioni, Abdukodir Khusanov katika dirisha hili akitokea Lens ambaye mpira wake wa kichwa uliompatia Noni Madueke bao la mapema.

Pep Guardiola hakuzungumza na Khusanov baada ya mechi kwa sababu fundi huyo kutoka Uzebekhstan hajui Kiingereza lakini alisema bado ni mchezaji mdogo hivyo, atajifunza.

“Bado ni mdogo sana. haikuwa rahisi kwake kucheza dhidi ya wachezaji hawa wazuri wa Chelsea, nilimfanyia mabadiliko kwa sababu ya kadi ya njano aliyokuwa nayo, si kwa sababu alisababisha goli.”