Mane kutua Ujerumani kesho

MUNICH, UJERUMANI. SADIO Mane atawasili Ujerumani kesho kwaajili ya kukamilisha uhamisho wake na atasaini mkataba wa kukipiga Bayern Munich baada ya kupima vipimo vya afya.
Mane, 30, atatambulisha Allianz Arena abada ya kukamilisha utaratibu wote wa ishu yake ya usajili iliyogharimu kitatu cha Pauni 35.1 milion.
Liverpool imepata pigo baada ya kumkosa Mane majira haya ya kiangazi, lakini uhamisho huo umekamilika haraka baada ya fowadi huyo wa Kimataifa Senegal, kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuicheza Anfield msimu ujao.
Mane alijiunga na Liverpool kwa kitita cha Pauni 31 milioni, na kuongeza kiasi kingine cha pesa Pauni 2.5 milioni na kukinukisha Anfield ndani ya miaka sita aliyokipiga.
Ndani ya miaka sita aliyocheza Anfield, Mane alfunga maabo 120 katika mechi 120 alizocheza mashindano yote, aidha katika mafanikio Kimataifa, fowadi huyo aliisaidia Senegal kubeba ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), yaliyofanyika mwaka huu.