Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Desabre: Tunafahamu DR Congo inadharauliwa, lakini tutapambana

DESABRE Pict

Muktasari:

  • DR Congo inatarajia rekodi hiyo thabiti itaisaidia katika mechi ya leo Jumapili, huku timu hiyo ikilenga kuchukua hatua kuelekea kutimiza ndoto iliyodumu kwa muda mrefu, kwani haijawahi kuonekana kwenye Kombe la Dunia tangu 1974, wakati nchi hiyo iliposhiriki kama Zaire.

Kocha wa mkuu wa timu ya taifa ya DR Congo, Sébastien Desabre, amekiri kuwa kikosi chake kinachukuliwa kama washindikizaji kuelekea mechi ya fainali ya mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, dhidi ya Nigeria, itakayopigwa leo Jumapili, Novemba 16, 2025.

DR Congo ilijihakikishia nafasi ya kucheza mechi ya fainali, baada ya kuichapa Cameroon bao 1-0, Novemba 13, 2025 katika Uwanja wa Prince Héritier Moulay El Hassan, huku Super Eagles ikiichapa Gabon 4-1.

Desabre mwenye umri wa miaka 49, ameizungumzia Nigeria kwa kusema nchi hiyo ina kikosi bora, hana budi kutoa heshima hiyo kutokana na jambo hilo kukubalika karibu kila kona ya Bara la Afrika kwa sasa.

Hata hivyo, kocha huyo raia wa Ufaransa, amesisitiza ubora wa Nigeria hauiondolei DR Congo sifa ya kuwa na timu ya kupambana, na hadi sasa anashangazwa kuona na kusikia mashabiki wanaitaja timu yake kama wasindikizaji.
 
“Ikumbukwe kuwa tumeifunga timu yenye ubora Cameroon, ambayo ilitengeneza nafasi nyingi ambazo zilihatarisha nafasi yetu ya kuwa hapa, lakini hiyo haikuturudisha nyuma, zaidi ya kupambana na kupata ushindi.

GER 01

“Tunaona na kusikia maneno ya DR Congo kutajwa kama timu msindikizaji kuelekea mechi yetu na Nigeria, hilo linatushangaza japo tunatambua wapinzani wetu wana ubora kuliko sisi, lakini jambo la msingi hapa tunakwenda kupambana na dhamira yetu ni kushinda,” amesema Desabre.

“Kwangu mimi ninaamini Nigeria na Cameroon ni timu zilizopo mbele yetu katika viwango vya FIFA, na tunajua bado tuna nafasi ya kuendelea kujiboresha hadi kufikia walipo wenzetu, na hili ndilo lionalosemwa zaidi kama kigezo cha sisi kuwa wasindikizaji kuelekea mechi yetu ya leo.”

Hata hivyo, Desabre ameonyesha imani kwa kikosi chake, kupitia maandalizi waliyoyafanya kwa ajili ya kuikabili Nigeria katika uwanja wa mapambano, baadae leo Jumapili.

CHELE Pict

“Hii itakuwa mechi nyingine, na tukio lolote litakalotokea, tutajitolea kikamilifu kwenye mchezo huo, kwa hakika tuna lengo la kutaka kuwa wawakilishi wa Afrika katika mechi za mwisho za mchujo ambazo zitashirikisha timu za amtaifa mengine duniani.”

Leopards imeshinda mechi tatu zao za mwisho kila moja kwa bao moja tu, ikionyesha timu inayofaidi zaidi mfumo imara wa ulinzi kuliko ushambuliaji, tofauti na ilivyo kwa Nigeria.

DR Congo inatarajia rekodi hiyo thabiti itaisaidia katika mechi ya leo Jumapili, huku timu hiyo ikilenga kuchukua hatua kuelekea kutimiza ndoto iliyodumu kwa muda mrefu, kwani haijawahi kuonekana kwenye Kombe la Dunia tangu 1974, wakati nchi hiyo iliposhiriki kama Zaire.