Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manchester United yatoa msimamo kuhusu Rashford

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Licha ya Barca kuonyesha nia ya kumbakisha Rashford, mabosi wa Old Trafford wameshikilia msimamo wakiamini thamani ya mchezaji huyo iko juu kutokana na uwezo aliouonyesha msimu huu Barcelona.

MANCHESTER United imesisitiza kuwa haina mpango wa kushusha bei ya Pauni 26 milioni iliyoiweka kwa mshambuliaji wa kimataifa wa England, Marcus Rashford, 28, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo  Barcelona.

Licha ya Barca kuonyesha nia ya kumbakisha Rashford, mabosi wa Old Trafford wameshikilia msimamo wakiamini thamani ya mchezaji huyo iko juu kutokana na uwezo aliouonyesha msimu huu Barcelona.

Hatma ya Rashford inatarajiwa kuamuliwa baada ya msimu kumalizika na inadaiwa Man United inataka Barca itoe Pauni 26 milioni ili kumnunua jumla, na ikishindwa kufanya hivyo itoe kiasi cha pesa kama ada ya kumchukua tena kwa mkopo pamoja na kuwa tayari kulipa mshahara wake wote wa msimu ujao.

Mkataba wa Rashford unamalizika 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu akiwa na Barca amecheza mechi 34 za michuano yote, akifunga mabao 10 na kutoa asisti 13. Rashford mwenyewe anatamani kuendelea kusalia Barca anakocheza kila mara.



Antonio Rudiger

TOTTENHAM Hotspur, Crystal Palace na West Ham United zimeonyesha nia ya kumsajili beki wa kimataifa wa Ujerumani wa Real Madrid, Antonio Rudiger, 32, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Rudiger amewahi kucheza England akiwa na Chelsea, jambo linalofanya timu hizo kuamini atazisaidia kwani hatakuwa mgeni. Madrid bado haijaweka wazi msimamo juu ya mustakabali wa beki huyo.


Julian Alvarez

ATLETICO Madrid inaendelea kufanya jitihada za kumbakisha mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Julian Alvarez, 26, kwa kumpa mkataba mpya mnono zaidi.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza Alvarez tayari ameonyesha hataki kusalia katika kikosi hicho kipaumbele kikubwa kwa sasa ni kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine. Taarifa zinadai anawindwa na Barcelona pamoja na Arsenal.


Wilson Isidor

SUNDERLAND inasaka straika mpya dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuziba pengo linalotarajiwa kuachwa na nyota wa kimataifa wa Ufaransa, Wilson Isidor, 25, ambaye ameonyesha nia ya kutaka kuondoka mwisho wa msimu.

Isidor anaripotiwa kutafuta changamoto mpya baada ya kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza. Uongozi wa Sunderland tayari unaandaa orodha ya washambuliaji mbadala.


Nick Woltemade

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ujerumani, Nick Woltemade, 24, anaripotiwa kutokuwa na furaha Newcastle United, jambo linalomfanya kuwa tayari kurejea Bundesliga ikiwa atapata ofa.

Kwa mujibu wa taarifa, Woltemade angependa zaidi kurudi katika klabu aliyowahi kung’ara ya Stuttgart, huku pia Bayern Munich ikitajwa kuwa chaguo lake lingine. Straika huyo anapata wakati mgumu kupata nafasi kikosini.


Nicolas Jackson

WAWAKILISHI wa mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya  Senegal, Nicolas Jackson, 24, wanatarajiwa kukaa mezani na mabosi wa Chelsea kutathmini mustakabali wake baada ya Bayern Munich kuonyesha kutokuwa tayari kumsainisha mkataba wa kudumu mwisho wa msimu.

Jackson ambaye yuko Ujerumani kwa mkopo wa msimu mzima, amekuwa hapati dakika za kutosha baada ya benchi la ufundi kutoridhishwa naye.


Ivan Toney

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Ivan Toney, 29, ambaye kwa sasa anakipiga Al-Ahli, amedai kuwa yupo tayari kurejea Ligi Kuu England ikiwa atapata ofa itakayomvutia.

Toney anadaiwa kuwa bado anahitaji kucheza soka la ushindani Ulaya na mwaka jana aliwahi kuhusishwa na Tottenham ambayo ilikuwa tayari kumsajili kabla ya kufeli kwa dili katika dakika za mwisho. Mkataba wa sasa wa staa huyo unatarajiwa kumalizika 2028.


Dominik Szoboszlai

LIVERPOOL haina mpango wowote wa kumuuza kiungo wa kimataifa wa Hungary, Dominik Szoboszlai, 25, licha ya taarifa zinazomhusisha na Real Madrid.

Inaelezwa uongozi wa Liverpool unaendelea na mazungumzo ya mkataba mpya kwa ajili ya nyota huyo ambaye unamtazama kama sehemu ya mipango ya muda mrefu.

Szoboszlai amekuwa na mchango mkubwa katika safu ya kiungo ya Liverpool na mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.