Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nico Williams aifungulia mlango Arsenal dirisha lijalo

Muktasari:

  • Williams amekuwa katika vichwa vya habari tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka juzi, ambapo alikuwa karibu kujiunga na Barcelona, lakini dili lilifeli na badala yake akasaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Athletic Bilbao.

MABOSI wa Arsenal, wamefanya mawasiliano na wakala wa  winga wa Hispania, Nico Williams, 23, na tayari wameambiwa kwamba staa huyo anataka kuondoka Athletic Bilbao katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Williams amekuwa katika vichwa vya habari tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka juzi, ambapo alikuwa karibu kujiunga na Barcelona, lakini dili lilifeli na badala yake akasaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Athletic Bilbao.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amevutiwa na kasi ambayo staa huyo ameionyesha, na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 26 za michuano yote akifunga mabao manne na asisti sita. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2035 na Athletic Bilbao inadaiwa itakuwa tayari kumuuza ikiwa Nico mwenyewe ataridhia kuondoka. Kwa mujibu wa vyanzo Williams anauzwa takribani Euro 100 milioni, kiasi ambacho Arsenal wanaweza kukitoa ingawa watafanya mazungumzo.


Alexis Mac Allister

MANCHESTER United inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya Argentina, Alexis Mac Allister, 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2022 anatajwa kuwa huenda akaondoka Anfield mwisho wa msimu ikiwa Majogoo watapokea ofa nono. Hata hivyo, dili hilo linaonekana kuwa na ugumu kukamilika kutokana na historia ya timu hizo mbili ambapo upinzani wa muda mrefu umefanya kuwa changamoto kuuziana hata wachezaji.


James Trafford

MANCHESTER  City inataka kumtoa kwa mkopo kipa wa kimataifa wa  England, James Trafford, 23, badala ya kumuuza kabisa katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Klabu kibao za England ambazo ni pamoja na Leeds United, Aston Villa na Newcastle United zinaonyesha nia ya kuhitaji huduma yake. Man City inaona kumtoa kwa mkopo ndio njia bora ya kumpa Trafford muda wa kucheza kwa kiwango cha juu. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2029.


Scott McTominay

MABOSI wa Napoli wamemuweka katika mpango wa kumbakisha kikosini kiungo wa kimataifa wa Scotland, Scott McTominay, 29, kama sehemu ya vipaumbele vya msimu ujao licha ya kuwepo kwa timu nyingi zinazomtaka. Klabu hiyo iko tayari kumpa mkataba mnono Scott ili aendelee kubaki katika kikosi kwa muda mrefu. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028. Klabu kadhaa za Ligi Kuu England zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili.


Nicolas Jackson

MSHAMBULIAJI wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal, Nicolas Jackson, 24, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Bayern Munich anatarajiwa kurejea Stamford Bridge dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika. Jackson atarejea Chelsea kwa sababu Bayern haionekani kuwa na mpango wa kumsainisha mkataba wa kuendelea kusalia katika kikosi chao baada ya kutoonyesha kiwango kilichotarajiwa.


Hakan Calhanoglu

GALATASARAY imeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Inter Milan na timu ya taifa ya Uturuki, Hakan Çalhanoglu, 32, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Hata hivyo, dili hilo linaonekana kuwa gumu kukamilika kutokana na umuhimu wa Calhanoglu katika kikosi cha Inter hususan msimu huu ambapo amefunga mabao saba katika mechi 17 za Ligi Kuu Italia.  Galatasaray inaamini uzoefu wake unaweza kuongeza nguvu katika safu ya kiungo.


Hayden Hackney

MANCHESTER United inaendelea kumfuatilia kwa karibu kiungo wa Middlesbrough, Hayden Hackney, 23, inayehitaji kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi. Hata hivyo, Mashetani Wekundu wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka Leeds United, Tottenham Hotspur na Everton ambazo zimeshaanza hadi mazungumzo na wawakilishi wake. Inaelezwa Man United inamtaka zaidi.


Nico Schlotterbeck

REAL Madrid inaonekana kuwa katika nafasi nzuri kumsajili beki wa kimataifa wa Ujerumani, Nico Schlotterbeck, 26, anayeichezea Borussia Dortmund. Hata hivyo, Barcelona wako vitani wakihitaji saini yake, jambo lililozua ushindani mkubwa ingawa Madrid inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili. Dortmund inadaiwa kuhitaji takribani Euro 50 milioni kwa ajili ya kumuuza Schlotterbeck.