Man United 'yapigwa kama ngoma'

NI MATESO. Usisikie, wikiendi iliyopita ilikuwa ngumu sana kwa mashabiki wa Manchester United baada ya timu yao kupokea kichapo cha mabao 6-3 katika mechi ya Manchester Derby iliyopigwa kweye dimba la Etihad.
Katika mchezo huo ulioanza saa 10:00 jioni Manchester City ilijipatia mabao yake kupitia kwa Erling Haaland na Phil Foden ambao wote walifunga hat-trick.
Hat-trick hizo zimesababisha Erling Haaland na  Foden, kuweka rekodi yakuwa wachezaji wawili waliofunga hat-trick kwenye mechi moja tangu 2019.
Mastaa wengine waliowahi kuweka rekodi hiyo ni  Jermaine Pennant, Robert Pires waliofanya hivyo kwenye mechi kati ya Arsenal dhidi ya  Southampton Mei 2003 kabla ya Ayoze Perez na Jamie Vardy kufanya hivyo kwenye mechi ya Leicester na Southampton, Oktoba 2019.
Mabao manne ya Man City yalipatikana katika kipindi cha ambapo Foden alifunga mawili dakika ya nane na 44, huku Haaland akifanya ivyo dakika 34 na 37.
Kipindi chapili Haaland alikamilisha hat-trick yake dakika ya 64 kabla ya Foden kufanya hivyo dakika ya 72 na mbali ya kufunga Haaland alitoa asisti mbil kwenye mechi hiyo.
Moja ya mambo yaliyoonekana ilikuwa ni muunganiko wake yeye na Kevin de Bruyne ambapo alipoulizwa Haaland kuhusu suala hilo alisema:"Mimi sijui muunganiko wetu unasababishwa nanini lakini nafikiri ni asili, tumejikuta tupo hivyo, hatukufanya mazoezi pamoja kwa muda mrefu sana kiasi cha kusema sababu hiyo, lakini hii hutokea na ninafuraha na hilo"
Haaland ameweka rekodi ya kufunga hat-trick ya tatu kwa muda mfupi zaidi akifanya hivyo kwenye mechi nane akiivuka rekodi ya Michael Owen ambaye alifanya hivyo kwenye mechi 48.
Matokeo hayo yameiwezesha Man City kufikisha alama 20 ikiwa nafasi pili huku Man United ikifikisha alama 12 kwenye nafasi sita.
Wakati mechi inaelekeza mapumziko mashabiki wa Man United wenye mioyo dhaifu walionekana wakitoka Uwanjani kwa kiwango kibovu cha timu yao.