Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yamtafuta anayevujisha siri zao

Muktasari:

  • Wachezaji Amad Diallo na Alejandro Garnacho wamehojiwa na Kocha Ruben Amorim endapo kama wanahusika kwenye jambo hilo.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imeanza uchunguzi wa kumtafuta mchezaji anayevujisha siri na mbinu za timu hiyo hadharani.

Wachezaji Amad Diallo na Alejandro Garnacho wamehojiwa na Kocha Ruben Amorim endapo kama wanahusika kwenye jambo hilo.

Kocha Amorim alisema baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City uwanjani Etihad, juzi Jumapili alisema hafurahishwi na kitendo cha taarifa za timu kabla ya mechi zao kufahamika mapema kabla ya wao kuzitambulisha rasmi, ikiwamo kikosi kinachoanza.

Amorim alisema: “Naijua hiyo stori, nadhani ni ngumu kumaliza hili tatizo, kwenye klabu kuna watu wengi sana, wachezaji wanazungumza na mawakala wao, sio kitu kizuri kabisa.”

Kocha Amorim ameshaonyesha bayana hatamvumilia mchezaji yeyote ambaye atakuwa na tabia za ovyo kwenye kikosi. Aliwaondoa kabisa kwenye kikosi chake kilichocheza na Man City, wachezaji Garnacho na Marcus Rashford kutokana na kutoonyesha utayari mazoezini.

Alisema mambo ya nje ya uwanja pia kama vile wachezaji wanavyokula, wanavyojihusisha na wachezaji wenzake pamoja na wanavyovaa katika kuelekea mchezo, hivyo ni vitu anavyovifanyia tathmini kabla ya kuchagua kikosi chake. Kwa kuanzia, kwenye mahojiano hayo, kocha Amorim ameshawishika si Amad au Garnacho waliohusika moja kwa moja kwenye uvujishaji wa siri za klabu nje.

Wakati Garnacho akitazama mechi ya Manchester derby nyumbani, Amad alikuwa shujaa wa Man United uwanjani Etihad.

Alisababisha penalti iliyoipa Man United bao la kusawazisha kwenye dakika 88 kabla ya kufunga bao la ushindi sekunde ya mwisho ya dakika 90 kabla ya zile dakika za majeruhi.

Amorim alimsifia Diallo baada ya mechi na kusema:

“Anaweza kucheza nafasi tofauti, ni kijana mtulivu. Yatupasa kuwa makini sana na Amad kwa sababu wakati mwingine kwenye klabu yetu tunawaweka makinda kwenye hali ya kujiona ni watu spesho sana. Acha tuwe watulivu kwa Amad.”