Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yaipora Chelsea tiketi ya Europa League

Muktasari:

  • Chelsea ambayo imemaliza nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu England ilikuwa na tiketi ya kucheza Europa League msimu ujao, lakini kwa kitendo cha Man United kubeba Kombe la FA, tiketi hiyo sasa imenyang’anywa na sasa itacheza kwenye Uefa Europa Conference League.

MANCHESTER, ENGLAND: BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Wembley, Manchester United imeitibulia Chelsea matumaini ya kucheza Uefa Europa League msimu ujao.

Chelsea ambayo imemaliza nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu England ilikuwa na tiketi ya kucheza Europa League msimu ujao, lakini kwa kitendo cha Man United kubeba Kombe la FA, tiketi hiyo sasa imenyang’anywa na sasa itacheza kwenye Uefa Europa Conference League.

Kanuni zinaeleza kwamba timu inayoshinda taji la FA England inafuzu kucheza Europa League kama haipo katika nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.

Kama timu bingwa wa ligi pia ni bingwa wa FA basi nafasi hiyo ya kushiriki Europa League itaangukia kwa timu iliyoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

Kwa kuwa Man United haikumaliza ndani ya Top Four kwenye msimamo ili kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo ushindi wa Kombe la FA imewapata tiketi ya kucheza Europa League.

Mabao ya Man United yamefungwa na Alejandro Gernacho dakika ya 30 kipindi cha kwanza kisha Kobbie Mainoo akapiga msumari wa pili dakika ya 39, bao la kufutia machozi la Man City likafungwa na Jeremy Doku dakika ya 87.

Hili linakuwa ni taji la 14 la FA kwa Man United na wapinzani wao Man City walikuwa wakilisaka taji hilo kwa mara ya nane