Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United wanafosi kumng’oa Bale Madrid

LISEMWALO lipo, ndiyo wanavyosema. Ni hivi, Manchester United wameripotiwa kumwambia Gareth Bale kulazimisha uhamisho wa kuhama Real Madrid ili wao wamchukue kama kweli anataka kurudi kwenye Ligi Kuu England kwenda kucheza Old Trafford.

Staa huyo wa kimataifa wa Wales amekuwa na wakati mgumu huko Santiago Bernabeu akipewa nafasi finyu za kuchezeshwa wakati kikosi hicho kilipokuwa chini ya kocha Mfaransa, Zinedine Zidane.

Bale, alianzia benchi hata kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyofanyika mwezi uliopita ambapo staa huyo alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 iliyopata Real Madrid dhidi ya Liverpool.

Baada ya mechi hiyo, staa huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur alisema anataka ahakikishiwe nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza kwa msimu ujao, kwani amechoka kuwekwa benchi mara kwa mara.

Wakati staa huyo akiripotiwa kusema hilo, kocha wa Man United, Jose Mourinho ameweka wazi anahitaji mshambuliaji mwenye kiwango cha dunia na wanamtazama Bale kuwa ni chaguo sahihi, lakini kwanza ni yeye mwenyewe akubali kuondoka Bernabeu.

Kwa mujibu wa OKDiario, Man United wapo tayari kutumia kiasi cha Pauni 176 milioni kupata huduma ya Bale.

Mwandishi wa habari Mhispaniola, Eduardo Inda alidai kwamba Man United wamemwambia Bale kuwasilisha barua ya kuomba kuhama kwenye kikosi cha Real Madrid ili wao wakamilishe yaliyobaki.

“Bale mwaka jana alitaka kuondoka, kulikuwa na ofa kutoka Manchester United na mwaka huu mambo hayo yamerudi tena kwenye maisha yake na wanachotaka ni kulifanya jambo hilo kuwa hadharani, aseme anataka kuondoka,” alisema Inda.