Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United kumtumia Ugarte dili la Gordon

Muktasari:

  • Baadhi ya taarifa zimefichua Man United inaweza kutumia mwanya wa Newcastle kumhitaji Ugarte ili kufanikisha mchakato wa kumsajili winga wa timu hiyo, Anthony Gordon.

NEWCASTLE United inapanga kuimarisha safu yao ya kiungo dirisha lijalo la majira ya kiangazi na inamwangalia staa wa Manchester United, Manuel Ugarte, 25, kama moja kati ya malengo yao.

Baadhi ya taarifa zimefichua Man United inaweza kutumia mwanya wa Newcastle kumhitaji Ugarte ili kufanikisha mchakato wa kumsajili winga wa timu hiyo, Anthony Gordon.

Mara kadhaa imekuwa ikiripotiwa Man United inatamani sana huduma ya Gordon, lakini kumekuwa na vipingamizi mbalimbali ikiwemo bei yake na ushindani kutoka kwa timu nyingine ikiwemo Man City.

Hata hivyo, kwa sasa mambo huenda yakawa rahisi kwa upande wao kwani wanaweza kumtoa Ugarte kama sehemu ya ofa kisha wakatoa pesa kiduchu kukamilisha dili hilo la Gordon.

Ugarte anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kukaba, kuharibu mashambulizi na kulinda safu ya ulinzi, jambo linalomfanya kuwa chaguo muhimu kwa Newcastle.

Inaelezwa Newcastle pia inataka kuongeza ushindani na ubora eneo la kiungo na wanaamini uzoefu mkubwa alionao Ugarte utachagiza sana hali hiyo.


Marc Casado

TOTTENHAM Hotspur na West Ham United zote zinaripotiwa kuwa katika mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa Barcelona, Marc Casado, 22,  dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Casado amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Barca. Mkataba wa sasa wa Casado unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote.


Eli Junior Kroupi

LIVERPOOL na Chelsea zitaingia vitani kuiwania saini ya mshambuliaji wa Bournemouth, Eli Junior Kroupi, 19, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Bournemouth ipo tayari kusikiliza ofa kutoka kwa timu zinazohitaji huduma ya staa huyu lakini kwa kiasi kisichopungua Pauni 60 milioni. Ushindani kati ya Liverpool na Chelsea juu ya staa huyu unadaiwa kuwa mkali sana na huenda thamani yake ikaongezeka maradufu. Mkataba wa sasa wa Kroupi unayatajiwa kumalizika mwaka 2030.


Joel Piroe

MSHAMBULIAJI wa Leeds United, Joel Piroe, 26, anaweza kuondoka katika kikosi hicho dirisha la majira ya kiangazi kutokana na kukosa muda wa kutosha kikosi cha kwanza. Ripoti zinaeleza Rangers inaonekana kuwa miongoni mwa vinara wa kutaka kumsajili nyota huyo, wakihitaji kuongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji. Piroe, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote.


Jeremy Monga

MANCHESTER United inapanga kufanya dili la kushtukiza la kumsajili winga Leicester City,  Jeremy Monga, 16, ambaye pia yupo katika rada za vigogo mbalimbali Ulaya ikiwemo Manchester City na Arsenal. Kwa mujibu wa tovuti ya Teamtalk, Man United ipo tayari kutoa hadi Pauni 25 milioni kuhakikisha inaipata huduma ya fundi huyu. Mkataba wa sasa wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Malik Tillman

FULHAM inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Bayer Leverkusen, Malik Tillman, 23, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Ripoti zinadai mabosi wa Fulham wanataka kumsajili Tilman ili akawe mbadala wa kiungo wao Harry Wilson ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na tayari timu kadhaa kubwa zimeonyesha nia ya kumsajili, hivyo nafasi ya kumbakisha kwa Fulham inaonekana kuwa ngumu


Zeki Celik

LIVERPOOL imepiga hatua kubwa katika mazungumzo yao ya kumsajili beki wa AS Roma na timu ya taifa ya Uturuki, Zeki Celik, 29, ambaye wakala wake ameweka wazi mchezaji huyo anataka kutafuta changamoto mpya nje ya Italia kwa msimu ujao.

Inaelezwa Liverpool wanamwona Celik kama chaguo sahihi la kuongeza ushindani upande wa kulia wa safu yao ya ulinzi. Maamuzi ya mwisho juu ya hatma ya fundi huyu yanatarajiwa kufanyika baada ya msimu kumalizika.


Hugo Bueno

NEWCASTLE United imefanya makubaliano binafsi ya kumsajili beki wa Wolves, Hugo Bueno, 23, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Bueno, ambaye ni raia wa Hispania, amekuwa akionyesha kiwango bora akiwa na Wolves licha ya timu hiyo kutofanya vizuri Ligi Kuu England msimu huu. Inaelezwa Newcastle sasa inataka kuingia makubaliano na Wolves baada ya kumalizana na upande wa Bueno ambao hauonekani kuwa na pingamizi.