Man United hiyooo....

Wednesday January 13 2021
man u pic

MANCHESTER, ENGLAND. HUKO Old Trafford ni kicheko tu, mara baada ya kufunga bao la ushindi wakati Manchester United inaichapa Burnley bao 1-0 na kupaa kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu England, Paul Pogba amesema yeye na wachezaji wenzake wataendelea kupambana hadi mwisho wa msimu bila ya kujali matokeo wanayoyapata.
Pogba aliingia kambani dakika ya 71 katika mechi hiyo iliyopigwa juzi, Jumanne na kuiwezesha Man United kukaa kileleni  kwa mara ya kwaza tangu Sir Alex Ferguson astaafu.
Baada ya kushinda Man United inakuwa imefikisha alama alama 36 nyuma ya bingwa mtetezi Liverpool, iliyo nafasi ya pili kwa alama 33.

man u pic 1


"Ilikuwa  ni ngumu sana kucheza nao na kuwafunga, wana wachezaji wakomavu sana, lakini tulionyesha utulivu na kupata bao, bado kuna safari ndefu hivyo tutapambana hadi mwisho wa msimu,"alisema.
Baada ya mechi Man United itakuwa inajiandaa kwa ajili ya kuumana na Liverpool Januari 17 saa 1:30 kisha itacheza na Fulham kabla ya kuwaalika tena Liverpool Januari 23.

Advertisement