Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United bado inamtaka Jean-Philippe Mateta

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Hatua hiyo inakuja baada ya dili la Mateta kuhamia AC Milan kufeli siku ya mwisho ya dirisha la usajili, jambo lililomfanya aendelee kubaki Selhurst Park.

MANCHESTER United inatajwa kufufua tena nia yake ya kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, 28, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hatua hiyo inakuja baada ya dili la Mateta kuhamia AC Milan kufeli siku ya mwisho ya dirisha la usajili, jambo lililomfanya aendelee kubaki Selhurst Park.

Man United ilianza kumwinda Mateta tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini dili lilifeli kutokana na kiasi cha pesa kilichohitajika na Palace. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Mateta alikuwa ameshafikia hadi makubaliano binafsi na Milan ambayo ili ilishafanya makubaliano na mabosi wa Palace, lakini changamoto ilionekana kwa kocha Oliver Glasner ambaye alizuia fundi huyo kuondoka hadi atakapopatikana mbadala wake.

Huyu sio mchezaji wa kwanza kuzuiwa Glasner kuondoka, aliwahi kufanya hivyo pia kwa Marc Guehi katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwenda Liverpool katika dakika za mwisho ambapo alisema angejiuzulu iwapo staa huyo angeondoka kwa sababu hakukuwa na muda wa kutafuta mbadala wake.

Msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote, amefunga mabao 10 na kutoa asisti mbili.


Dusan Vlahovic

AC MILAN, Chelsea na Newcastle United zinaripotiwa kumfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic, 26, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Fundi huyu alitajwa kuwa huenda akaondoka katika dirisha lililopita la majira ya baridi ambapo timu nyingi kutoka England zilionyesha nia ya kumsajili, lakini ilishindikana baada ya kupata jeraha ambalo litamweka nje hadi mwezi ujao.

Hadi sasa hakuna mazungumzo ya mkataba mpya kati yake na mabosi wa Juventus na anatajwa kuwa na asilimia nyingi za kuondoka akiwa huru mwisho wa msimu.


Adam Wharton

LIVERPOOL inaweza kuingia kwenye vita ya usajili dhidi ya Manchester United na Real Madrid kuiwania saini ya kiungo wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Adam Wharton, 21.

Ripoti zinaeleza Palace ipo tayari kusikiliza ofa kuanzia pauni 80 milioni kwa ajili ya kumuuza fundi huyu katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Wharton anaonekana kuwa mmoja kati ya viungo vijana wanaowindwa zaidi barani Ulaya kwa sasa. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Sandro Tonali

MANCHESTER UNITED inaendelea kupanga maboresho makubwa kikosini na sasa inamwangalia kiungo wa Newcastle United na Italia, Sandro Tonali, 25.

Ripoti zinaeleza United inataka kuongeza ubora, uzoefu na nguvu katikati ya uwanja, huku Tonali akionekana kuwa chaguo linalolingana na mipango yao ya muda mrefu.

Hata hivyo, Newcastle hawako tayari kumuachia kirahisi kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi.


Dwight McNeil

EVERTON ipo tayari kusikiliza ofa mpya kwa ajili ya winga wake raia wa England, Dwight McNeil, 26, baada ya dili lake la siku ya mwisho ya dirisha la usajili  kuhamia Crystal Palace kufeli.

McNeil anatajwa kutaka changamoto mpya, huku Palace ikiendelea kuwa kati ya klabu zinazoweza kurejea mezani mwisho wa msimu.

Mkataba wa sasa wa McNeil unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Everton na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote.


Patrick Zabi

NEWCASTLE UNITED inapanga kufufua tena nia yake ya kumsajili kiungo kinda wa Reims mwenye kipaji kikubwa, Patrick Zabi, 19, mwisho wa msimu huu.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji vijana wenye vipaji vikubwa nchini Ufaransa kwa sasa.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 21 za michuano yote, amefunga mabao mawili na kutoa asisti tatu.


Illan Meslier

LEEDS UNITED huenda ikampoteza kipa wake namba moja, Illan Meslier, 25, kwenda klabu ya Besiktas ya Uturuki baada ya kuanza mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumuuza.

Ripoti zinaeleza kuwa Meslier yuko tayari kuondoka na amevutiwa sana na mpango wa Besiktas kutaka kumsajili na anaona itakuwa ni jambo zuri kupata changamoto mpya.

Licha ya kwamba haitokuwa na uwezo wa kutafuta mbadala wake Leeds inaripotiwa kuwa tayari kumuuza kipa huyu baada ya kuona anauhitaji sana wa kuondoka.


Leon Goretzka

KIUNGO wa kimataifa wa Ujerumani, Leon Goretzka, 30, ambaye mkataba wake na Bayern Munich unamalizika mwisho wa msimu, anaweza kujiunga na Arsenal bure katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Benchi la ufundi la Arsenal, linaamini Goretzka atasaidia sana katika safu yao ya kiungo kwa kuongeza uzoefu katika eneo hilo.

Staa huyu ameshinda mataji kadhaa na Bayern Munich. Akiwa na Bayern msimu huu amecheza mechi 28 za michuano yote.