Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United, Arsenal nani kutinga bila gadi Old Traffod!

Muktasari:

  • Manchester United, nafasi ya nane kwenye msimamo. Mechi 35, pointi 54. Kwenye mechi hizo, imeshinda 16 tu, sare sita na vichapo 13. Ndiyo, vichapo ni Kumi na Tatu.

MANCHESTER, ENGLAND: NAMBA hazidanganyi. Ukitazama tu, namba zinavyosoma unapata picha, nani anapigwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Manchester United, nafasi ya nane kwenye msimamo. Mechi 35, pointi 54. Kwenye mechi hizo, imeshinda 16 tu, sare sita na vichapo 13. Ndiyo, vichapo 13.

Imefunga mabao 52, imefungwa mabao 55. Hivyo, ina -3 ya tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Inadaiwa mabao matatu, kwa sababu imefungwa mengi kuliko iliyofunga.

Leo, Jumapili timu yenye rekodi hizo, itacheza na Arsenal uwanjani Old Trafford. Itakabiliana na Arsenal, ambayo yenyewe ipo kwenye mbio za kufukuzia ubingwa.

Arsenal imecheza mechi 36. Imevuna pointi 83. Katika mechi hizo, imeshinda 26, tofauti ya mechi 10 na Man United. Imetoka sare tano na ipoteza tano tu. Imefunga mabao 88 na imefungwa 28, hivyo ina +60 ya tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Tofauti ya pointi za Arsenal na Man United ni 29. Namba zinajieleza, kwa msimu huu, ubora wa uwanjani kati ya Man United na Arsenal ni ardhi na mbingu. Kuna cha kuitisha Arsenal kweli kwenye vita yake ya kusaka ubingwa?

Kwa takwimu hizo, huwezi kushawishika kuweka shilingi yako upande wa Man United. Italiwa.

Viwango vya kila timu kwa mechi tano zilizopita. Man United kwenye mechi tano za mwisho ilizocheza kwenye Ligi Kuu England, imeshinda moja, imechapwa moja na kutoka sare tatu.

Mchezo wa hivi karibuni, iliokota mipira kwenye nyavu zao mara nne kwenye kichapo cha 4-0 dhidi ya Crystal Palace. Arsenal yenyewe kwenye mechi tano za mwisho, imeshinda nne, imepoteza moja. Mechi nne za mwisho imefunga mabao 13 na kufungwa mawili tu. Man United mechi nne za mwisho, imefungwa mabao tisa na imefunga saba. Man United ya msimu huu imecheza mechi nane tu ndizo ambazo haijaruhusu nyavu zao kuguswa, wakati Arsenal imecheza mechi 17 bila ya nyavu za kuguswa.

Takwimu za jumla, Man United na Arsenal zimekutana mara 63 kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England. Kwenye mechi hizo, sare ni 18. Man United imeshinda 26, mara 18 nyumbani na nane ugenini, wakati Arsenal yenyewe imeshinda 19, mara 15 nyumbani na nne ugenini. Kinachoipa matumaini Man United ni rekodi yao ya Old Trafford inapocheza na Arsenal kwenye mechi za Ligi Kuu England. Kwenye uwanja huo katika mechi ya ligi, Arsenal katika mechi 10, imeshinda moja tu. Ushindi wa Arsenal uwanjani hapo, ilikuwa Novemba 1, 2020. Sare nne na vichapo vitano. Pengine hicho ndicho ambacho Man United inatambia kuhusu Arsenal wakati wakienda Old Trafford kukipiga kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu England. Kitakwenda kutokea nini leo huko Old Trafford. Shughuli ni saa 12:30 jioni.