Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yaja na mbinu kali kumnasa Sandro Tonali

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Taarifa zinadai Man City inataka kuongeza nguvu katika safu ya kiungo, na inamuona Tonali kuwa chaguo sahihi baada ya kiwango bora alichoonyesha msimu huu kuanzia klabuni hadi timu ya taifa ya Italia.

MAN City ipo tayari kutoa baadhi ya wachezaji kama sehemu ya dili la kuishawishi Newcastle United kuiuzia kiungo Sandro Tonali, 25, dirisha la kiangazi.

Taarifa zinadai Man City inataka kuongeza nguvu katika safu ya kiungo, na inamuona Tonali kuwa chaguo sahihi baada ya kiwango bora alichoonyesha msimu huu kuanzia klabuni hadi timu ya taifa ya Italia.

Hata hivyo, bado haijafahamika kama Newcastle itakubali mpango huo kutokana na umuhimu wa Tonali ndani ya kikosi chake.

Mbali ya Tonali, Man City pia inahitaji huduma ya kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson ili kuziba mapengo ambayo huendwa yakaachwa na Rodri na Bernado Silva.

Rodri anaonekana kuwa na asilimia kubwa kutimkia Real Madrid ambayo imekuwa ikihitaji saini yake kwa muda mrefu, huku Silva hadi sasa hatma yake haijajulikana ambapo baadhi ya taarifa zinadai anaweza kuondoka mwisho wa msimu mkataba wake utakapomalizika. Newcastle haionekani kuwa tayari kumwachia Tonali, na hata ikimwachia itahitaji pesa nyingi.


James Trafford

NEWCASTLE United bado ina nia ya kumsajili kipa wa kimataifa wa England, James Trafford, 23, kutoka Manchester City. Inaelezwa kuwa Newcastle imeongeza juhudi ya kutaka kumsajili baada ya kuibuka kwa taarifa zinazodi Trafford anataka kuondoka ili kutafuta nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.Kipa huyo mkataba wake wa sasa na Man City unatarajiwa kumalizika 2030 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 13.


Evan Ndicka

TIMU kadhaa Ulaya ikiwemo Barcelona, Tottenham Hotspur, Liverpool na Manchester United zinafuatilia kwa karibu hali ya beki wa AS Roma, Evan Ndicka, 26.

Inaelezwa Roma iko tayari kusikiliza ofa zinazoanzia Pauni 39 milioni kwa ajili ya beki huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye ameonyesha kiwango bora katika Serie A msimu huu. Kutokana na ushindani mkubwa wa kuwania saini yake, huenda bei hiyo ikaongezeka maradufu hadi kufikia Pauni 60 milioni.


Roggerio Nyakossi

LIVERPOOL na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazomuwania beki wa kimataifa wa Uswisi, Roggerio Nyakossi, 22, kuelekea dirisha lijalo. Nyakossi ambaye kwa sasa anakipiga OH Leuven yupo mwaka wa mwisho wa mkataba wake jambo lililosababisha hata bei yake kuwa ndogo na kuvutia klabu nyingi. Hadi sasa hakuna timu inayoonekana kuwa na nafasi kubwa kwani mazungumzo bado yanaendelea. Msimu huu amecheza mechi 20.


Marcos Llorente

KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Marcos Llorente, 31, ameweka wazi kuwa anataka kuendelea kubaki katika kikosi cha  Atlético Madrid. Inaelezwa Llorente yuko kwenye mazungumzo ya  mkataba mpya na klabu hiyo, licha ya hapo awali ripoti kueleza kwamba anawindwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu England. Uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali umeifanya Atletico kutokuwa tayari kumwachia kirahisi.


Adam Wharton

REAL Madrid ni miongoni mwa klabu zinazomuwania kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton mwenye umri wa miaka 22, ili kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa Wharton aliye katika kiwango bora katika kikosi cha Palace tangu msimu uliopita amekuwa akifuatiliwa na maskauti wa Madrid kwa muda mrefu na wameonekana kuridhishwa na kiwango chake. Wharton anaonekana kutamani dili likamilike.


Nico Schlotterbeck

BEKI wa kati wa kimataifa wa Ujerumani, Nico Schlotterbeck, 26, yupo karibu kusaini mkataba mpya wa kusalia Borussia Dortmund hadi 2031. Inaelezwa Dortmund imefanikiwa kumshawishi kusaini licha ya Liverpool na Real Madrid kuonyesha nia ya kumtaka.

Schlotterbeck ameendelea kuwa nguzo katika safu ya ulinzi ya Dortmund, na klabu hiyo inaonekana kuwa tayari kumlinda kwa nguvu zote.


Noah Atubolu

TOTTENHAM Hotspur imeanza mazungumzo ya kumsajili kipa wa Freiburg na Ujerumani, Noah Atubolu, 23, katika dirisha lijalo la la majira ya kiangazi baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu na kuridhishwa na kiwango chake.

Hatua hiyo inakuja wakati kipa namba moja, Guglielmo Vicario, akidaiwa kuwa katika mpango wa kurejea Italia, ambapo Inter Milan inaonekana kutaka kumsajili hivyo inahitaji akawe mbadala.