Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yailiza Madrid nyumbani kwao

Muktasari:

  • Alonso yuko chini ya shinikizo kubwa kufuatia mwenendo mbaya kwenye ligi pamoja na madai ya kutofautiana kitabia na baadhi ya wachezaji wa Madrid, na matokeo haya yatazidisha moto baada ya kikosi chake kushindwa kulinda uongozi wa mapema.

MADRID, HISPANIA: Manchester City imepindua matokeo kutoka kuwa nyuma na kupata ushindi wa mabao 2-1 kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid, ambao ni mabingwa wa kihistoria wa mashindano hayo, na kumwacha kocha wa Los Blancos, Xabi Alonso, akiwa katika hatihati ya kupoteza kibarua chake.

Alonso yuko chini ya shinikizo kubwa kufuatia mwenendo mbaya kwenye ligi pamoja na madai ya kutofautiana kitabia na baadhi ya wachezaji wa Madrid, na matokeo haya yatazidisha moto baada ya kikosi chake kushindwa kulinda uongozi wa mapema.

Madrid ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Kylian Mbappé, kuruhusiwa kukaa benchi pekee kutokana na kutokuwa fiti vya kutosha. Nahodha huyo wa Ufaransa hakushiriki hata dakika moja huku wenzake wakipoteza mechi hiyo iliyochezwa nyumbani kwao Santiago Bernabeu, usiku wa Desemba 10, 2025

City ilikaribia kuanza vibaya kufuatia Matheus Nunes kumwangusha Vinícius Jr ndani ya dakika za mwanzo, na mwamuzi akaamuru penalti. Hata hivyo, baada ya kupitia VAR, adhabu hiyo ilibadilishwa na kuwa faulo pembeni ya eneo la hatari. Federico Valverde alikaribia kufunga kupitia mpira huo wa adhabu lakini shuti lake lilipanguliwa kidogo na kupita pembeni, huku Vinícius naye akikosa kwa kidogo alipodokoa mpira uliokwenda nje ya lango.

City ilionekana kutuliza mchezo na kumiliki mpira, lakini ikashitukizwa kwa kushambuliwa kwa kushtukiza pale Rodrygo Goes alipounganisha krosi ndefu ya Jude Bellingham na kufunga bao lake la kwanza tangu Januari 2025.

Hata hivyo, City ilirejea mchezoni dakika saba tu baadaye kupitia nafasi yao ya kwanza ya wazi, beki chipukizi Nico O’Reilly akipachika mpira wavuni baada ya kichwa cha Josko Gvardiol kurudishwa eneo la hatari na Thibaut Courtois.

Timu hiyo ya England iliongeza bao la pili kabla ya mapumziko kupitia penalti ya Erling Haaland baada ya kufanyiwa madhambi na Antonio Rüdiger ndani ya eneo la hatari. City ingeweza kuongeza bao la tatu, lakini Courtois alifanya kazi nzuri kuzuia jaribio la Haaland.

Kipindi cha pili Real Madrid ilitafuta kusawazisha kupitia Bellingham aliyepiga "chip" iliyopaa juu ya lango, na kijana Endrick ambaye mpira wake wa kichwa uligonga mwamba. Licha ya jitihada hizo, City ilidumu na uongozi hadi mwisho na kupata ushindi huo ugenini.